ASENGA MBUNIFU WA JIKO LA KIKAPU
Deograsias Asenga akiwa ameshika jiko la kikapu pamoja na malighafi inayotumika kutengeneza jiko hilo.
Peter Akaro
BADO watanzania wanashahuku ya kubuni vitu ambavyo vitainuisha
jamiii na kuiletea unafuu wa maisha kwa siku
za usoni.
Leo tupoona kijana Deograsias Asenga ambaye amebuni jiko
la kikapu ambalo linalitumia joto kiasi la sufuria kuivisha chakula.
Jiko hili linapika kwakutumia joto pekee yake ambalo
sufuria hutokanalo wenye moto wa awali ambao unaweza kuwa wa kuni, mkaa, umeme na hatagasi.
Kabla ya kufikambali zaidi ningependa tuangalie jinsi
jiko hilo linavyotengezwa ilikupata picha ya kile nina chozungumzia.
Asenga anasema kwanza unatakiwa kuwana kikapu ambacho
kinaweza kuwa cha mianzi au ukili,kitamba cheusi na malighafiya ‘Styrofoam’.
“Hizi malighafi hutumika kubebea runinga, redio, na vifaa
vya kieletroniki ambazo tunakuwa tumeshazisaga, kisha zinachanganywa na mafuta ya
kikapu na zikishalowa tunaanika kwa muda wa dakika 20.
Anasema baada ya hapo unaziingiza kwenye karatasi ambazo
ni laini sana kisha unaziingiza ndani ya kikapu ambapo ile karatasi itatakiwa izunguke
kikapu chote na kila sehemu kuwena hizo‘Styrofoam’.
“Hili karatasi inauzwa sh. 2,000, unakuja kuikata vipande
vipande kwa kulingana na ukubwa wa kikapu, mwishoni unashikilia kwa nje ili kupata
nafasi ya kuja kuingiza zile malighafi kwa uwiano.
Ukisha maliza unachukua kilekitambaa cheusi unashonea
juu lilekaratasi, ukishamaliza unakunja kisha unashonea ili kuondoa ule muonekano
wa kipapu cha ukili au mianzi.
Asenga anasema anaweka kitambaa cheusi kwasababu
kina uwezo wa kuakisi na kuifadhi joto kiurahisi.
Baada ya hatua hiyo inafuata utengenezaji wa ufuniko
wa jiko ambao unachukua mfuko wa nailoni
(malboro), kisha unasaga tena‘Styrofoam’na kuzichanganya na yale mafuta, baada ya hapo unaziweka ndani ya huo mfuko na kuushona.
“kuuchukua huu mfuniko kama ulivyo na kuuweka juu ya
jiko nikitu ambacho haikiwezekani, kwa hivyo unachukua kitambaa cheusi na kukishona,
kisha unashusha ule mfuko na kuingiza ndani yake na baadae unakuja kushona lile
eneo ulilopitisha ule mfuko.
“Hadi kufikia hapa jiko linakuwa tayari kutumika bila
shida yoyote,” anasema.
Jinsi
lina vyotumika
“Hili jiko linatengemea jiko lingine ambalo litaipa sufuria
joto na kile kilichopo ndani kwa muda ndipo ile sufuria ina hamishiwa huku ili kuendelea,
kwa mfano unapika ubwabwa, unachemsha maji katika jiko lingine na kuweka vitu vyote
vinavyohitajika baada ya muda unatoa kwenye
lile jiko la mwanzo, na kuweka kwenye kapu lako ambalo sasa ndio jiko na kufunika
na baaada ya dakika 20 ubwabwa wako utakuwa
umeivakabisa,” anasema.
Anasema jiko hili lina weza kuhifadhi joto kwa masaa
nane hadi 12, na mtu anaweza kutembea nalo huku anapika bila shida yoyote.
“Kama unapika maharage, utayachemsha kwenye jiko la
awali kwa dakika 30, baada ya hapo utaamishia kwenye jiko la kikapu na baadae ya
lisaa limoja na dakika 20 maharage yana kuwa yameiva vizuri na kulainika.
“Na unapokuwa umeweka maharage yakondani, ukisikiliza
kwanje utasikia kamajiko linatoamtetemeko kwasababu joto kwa asilimia kubwa linakuwa
limemezwa na zile malighafi na nailoni na mvuke unaendelea kubaki ndani nakuendelea
kuivisha.
“Mvuke hauwezi kuharibu kitambaa kwasababu hizimalighafi
zinahifadhi joto na kuachia kidogo kidogo,” anasema.
Anasema ‘Styrofoam’ zinapokuwa zinachanganya na mafuta
huwa zinatabia ya kufyonza na kutanuka, ila zinapokuwa zina chomwa najoto la
sufuria zinaachilia na kuwa ndogo zaidi, hivyo kuleta kuwana uwezo mkubwa zaidi
wa kupika na joto linapokuwa linazidi zinakuwa kama gundi.
Asenga anaongeza kuwa baadae zikipoa zinarudia katika
hali yake ya kawaida.
“kinachofanya kazi asilimia kubwa ni haya mafauta,
na ukitumia bila mafuta jiko litapika lakini halitakuwa na ubora …litapika kwa siku
kadhaa ingawa hili jiko linaweza kukaa zaidi ya miaka 10,” anasema.
Mafanikio na ushauri
Asenga anasema mwaka jana yeye na wenzake walichukuliwa na serikali hadi Mtwara katika kijiji cha Nanyambe kufundisha watu namna ya kutengeneza jiko la kikapu.
Anaongeza kuwa haikushia hapo bali walienda hadi Lindi Mjini ambako kulikuwa na maonyesho ya Nane Nane na hapo wakawafundisha watu pia.
“Ingawa walitusifu kwa kufanya kazi nzurii ila bado mchango wetu haujatambuli wa rasmi na serikali, bado kuna mlologo mrefu hadi kutufikia.
“Kwa mfano sisi tulipelekwa na Halimashauri ambao wangetakiwa kukaa nasisi kwasababu wao ndio wanajua kiu ya wananchi ni nini na watusaidie ili tuweze kujikwamua kiuchumi, si hadi kuongoja serikali kuu,” anasema.
Mbunifu huyu anasema huu ndio wakati ambao serikali ingetakiwa kuwasaidia kwasababu wameshaona uwezo wao hata kwa kufundisha wengine, na endapo likitekelezwa hilo nirahisikwa wao kuboresha na kubuni zaidi.
Wasifu wake
Anasema kiwango chake cha elimu ni darasa la saba ambapo alihitimu elimu hiyo mwaka 1997 katika Shule ya UaRombo Kilimanjaro.
“Baada ya hapo wakati nikisubiri matokeo nikajiunga na shule ya ufundi Mahida Rombo, na matokeo ya darasa la saba yalipotoka hayakuwa mazuri hivyo nikaamua kuja Dar es Salaam.
“Mwaka 1999 nikanza kufanya biashara ya vya kula hadi 2007, na mwaka uliofuata nikaanza tena shule ya ufundi wa magari katika Chuo fulani na mwaka 2009 ni kaenda kujiunga naVeta Chang”ombe ambapo ni liihitimu mwaka huo huo,” anasema.
Mbunifu huyu anasema ufundi wake uliishia daraja la pili kwa kuwa alishindwa kufaulu mitihani ya kujiunga na daraja la kwanza.
“Baada ya hapo nikawa nafanya kazi kwenye gereji lakini kazi zikawa hamna fedha ninayo pata haitoshi matumizi ya kifamilia.
“Lakini baadae nikaona hapana, nikaamua kujiingiza katika ubunifu na ujasiriamali ambao ndio unaendesha maisha yangu hadi sasa,” anasema.
Contact: 0755 299596
Comments
Post a Comment