VICTOR MUNENI, MWENYEKITI ALIYEDHUBUTU KUWAJENGEA OFISI MTAA WA SEA VIEW.

Na Enles Mbegalo

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Sea View, Victor Muneni, ameelezea jinsi alivyofanikiwa kujenga ofisi ya mtaa wake, ambapo awali hakukuwa na ofisi kwenye mtaa huo tangu kuanzishwa kwa serikali za mitaa.

Akizungumza na mwandishi wa blog hii leo jijini Dar es Salaam katika ofisi hiyo mpya, ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi ujao, Muneni alisema mtaa huo haukuwa na ofisi na alikuwa analazimika kuwafuata wananchi nyumbani kwaajili ya kutoa huduma.

Pia,  alisema alikuwa analazimika kutembea na mihuri kwenye mfuko ili wananchi watakapo mpigia simu na kuhitaji huduma kwenda moja kwa moja na sio kurudi nyumbani tena kwaajili ya kufuata mihuri hiyo.

 Aliongeza kuwa alilazimika  kutumia group la WhatsApp pamoja na vipeperushi  kwaajili ya kutoa taarifa za  shughuri za maendeleo ya mtaa.

“Mtaa wangu ulikuwa hauna ofisi, ila nashukuru Mungu nimeweza kupambana na kufanikiwa kujenga ofisi hii ambayo tunatarajia ikikamilika ianze kutumika mwezi wa sita,”alisema Muneni na kuongeza kuwa.

“Nilikuwa nalazimika kuwafuata wananchi nyumbani kwaajili ya kutoa huduma na  muda wote nilikuwa na tembea na mihuri kwenye mfuko  wangu wa suruali kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi,”

Muneni alisema ofisi hiyo ni ya kwanza tangu zilipoanzishwa serikali za mitaa, kwani mtaa wao haukuwahi kuwa na ofisi.

Alisema baada ya kuona ugumu wa kufanya kazi bila kuwa na ofisi ya mtaa alilazimika kuwafuata Shirika la Nyumba(NHC), Bank M, Hospitali ya Aga khan na wananchi na kuwaeleza shida ya mtaa wao  wa kutokuwa na ofisi.

“Nashukuru Mungu  nilipowaeleza walinielewa na walionyesha ushirikiano na hadi tumeweza kujenga ofisi hii ambayo ndio ya kwanza kwenye mtaa wetu tangu zilipoanzishwa ofisi za serikali za mitaa,”alisema

Pia Mwenyekiti huyo aliwashukuru sana wananchi wa mtaa wake pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza kuchangia ujenzi wa ofisi hiyo.

Muneni alisema licha ya kujenga ofisi hiyo ana mipango mbalimbali kwaajili ya kuboresha mtaa wake, ikiwa ni pamoja na kuboresha bustani kwenye barabara, ili kupendezesha madhari na kutunza mazingira.

“Nimeshaanza kuboresha bustani kwenye barabara ya Obama, kupanda miti katika barabara ya Ally Hassan Mwinyi, Mtaa wa Luhinda pamoja na kuweka taa barabara ya Sea View,”alisema  na kuongeza


“Mipango mingine ambayo tumeshaaza kutekeleza ni pamoja na kutengeneza bustani, kupanda miti na maua, kupanda majani, kuweka taa kwenye barabara za mitaa ili kuimarisha usalama zaidi, kuboresha Shule ya Msingi Bunge pamoja na kuweka njia kwa waenda kwa miguu,”


 Hii ni Ofisi Mpya ya Serikali ya Mtaa  wa Sea View ambayo imejengwa kwa juhudu za Mwenyekiti wa Mtaa huo, Victor Muneni, kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa huo na wadau mbalimbali na ikumbukwe kuwa mtaa huo haujawahi kuwa na ofisi ya mtaa tangu kuanzishwa kwa serikali ya mtaa huo.

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea View, Victor Muneni akiwa na Mjumbe wa ofisi hiyo, anayefahamika kwa jina la Mama Mussa, wakiwa wamesimama kwenye bango la ofisi yao leo.

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea View akizungumza jambo na Mjumbe wa ofisi hiyo Mama Mussa leo, wakati walipokuwa wakizungumzia juhudi zao za kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo mpya ambayo, ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika.

 
 Hii ni sehemu ambayo itatumika kwaajili ya mikutano katika ofisi hiyo.

 Mwenyekiti, Muneni akimuonyesha mwandishi wa blog hii, moja ya kiti kitakachotumika kwaajili ya watu wenye ulemavu.

 Mjumbe wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Sea View, Mama Mussa akionyesha sehemu ambayo itatumika kwaajili ya kubandika matangazo mbalimbali.

 
 Hii ni Sehemu ambayo itatumiwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo kwaajili ya kufanya shughuri zake za kiofisi.

Hii ni sehemu ambayo itatumiwa na Afisa Mtendaji kwaajili ya kufanya shughuri zake za kiofisi.

(PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG).

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.