MKURUGENZI MKUU WA NBS AFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI WA OFISI HIYO, NA KUWATAKA KUFANYA KAZI KWA BIDII.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kikao
cha wafanyakazi wa ofisi hiyo, kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee
jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Dkt.Chuwa amewataka wafanyakazi hao
kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu
rasmi nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala, Fedha
na Masoko, Lilian Karumuna wa Ofisi ya Takwimu akifafanua jambo
wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo, kilichofanyika leo katika ukumbi
wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania Tawi la Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (TUGHE) Raya Mikidadi akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa
ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Ofisi ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi
Mkuu Dkt. Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo, kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Ofisi ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi
Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).
Comments
Post a Comment