SERIKALI IMEOMBWA KUZIACHA TAASISI ZA DINI KUTOA HUDUMA KWA UTARATIBU WALIOJIWEKEA.
Na Mwandishi Wetu, Iringa.
SERIKALI imeombwa kuziacha Taasisi za dini
kuendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwamo elimu na afya kwa utaratibu
waliojiwekea badala ya kuzilazimisha kusajili na kuendesha huduma hizo kibiashara
jambo ambalo ni kinyume na malengo ya taasisi hizo.
Rai hiyo imetolewa juzi
na Paroko wa Parokia ya Nyabula Jimbo la Iringa, Padre Emil Kindole, kwenye
kongamano la vijana wa Vikaria ya Consolata lenye jumla ya parokia 11 kutoka
jimbo la Iringa.
Kindole alisema kuwa
“serikali inawaumiza pale ambapo inatutaka sisi kama kanisa tufanye biashara, hatujazoea biashara
wala biashara hatuijui kwa mfano St.Thomas iwe ni biashara tukate leseni ya biashara sisi
hatuwezi afya na shule ni huduma ukisema ni biashara lazima tukae upya
tujipange na tuseme tutaiendeshaje kibishara.”alisema Padri Kindole.
Naye Pascal Mahondo ambaye ni katibu wa Vikaria ya Consolata
alisema kuwa kongamano hilo limewekwa kwa lengo ya kuwaamsha
vijana kufanya uenezi wa injili takatifu kazi iliyoasisiwa na wamisionari
kutoka ulaya miaka150 iliyopita ambapo vijana wametakiwa kuwa mstari wa mbele
katika kuihubiri injili ili kuhakikisha taifa linaendelea kuwa na amani ambayo
ni kichocheo cha maendeleo.
Kwa upande wake mgeni
rasmi wa kongamano hilo ambaye ni Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rita Kabati alisema wabunge wa mkoa wa Iringa
wameanza kushughulikia changamoto ya za miradi ya huduma za mashirika ya dini
ili kuhakikisha huduma hizo zinaendelea kuwapo kwa lengo la kuisaidia jamii
kama ilivyo dhamira ya mashirika hayo.
Comments
Post a Comment