NBS YAKUTANA NA WATAALAM WA MFUMO WA TAARIFA ZA KIJIOGRAFIA (GIS) UTAKAOTUMIKA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKUSANYAJI TAKWIMU MBALIMBALI NCHINI.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina ya
wataalam kutoka Kampuni ya esri-
inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia
(GIS), walipokutana leo Jijini Dar es Salaam ili kujadili namna mfumo huo
unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.
Kulia ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirila la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA Tanzania) Dkt. Hashina Begum.
Mtalaam
kutoka kampuni ya esri - inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa
za Kijiografia (GIS), Bi. Linda Peters akielezea jambo wakati wa kikao baina ya
wataalam kutoka Kampuni hiyo na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni wataalam
kutoka Kampuni hiyo Bw. Patrick Kipchumba na Mhandisi Anthony Gakobo.
Baadhi ya wataalam
kutoka Kampuni ya esri - inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa
za Kijiografia (GIS), wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) walipokutana leo Jijini Dar es
Salaam ili kujadili namna mfumo huo unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la
ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.
Mtalaam wa Mfumo wa
Taarifa za Kijiografia (GIS) Anthony Gakobo akionyesha moja ya kifaa
kinachotumika katika kuhakiki uhalisia wa taarifa za kijiografia mbele ya
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), leo jijini Dar es Salaam. Kutoka
kushoto ni watalaam wa mfumo huo Patrick Kipchumba na Linda Peters.
Mshauri wa Masuala ya
Kitakwimu kutoka Benki ya Dunia – Tanzania, Elizabeth Talbert akifafanua
jambo wakati wa kikao cha pamoja baina ya wataalam kutoka Kampuni ya esri- inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo
wa Taarifa za Kijiografia (GIS) na menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) ili kujadili namna mfumo huo unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la
ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa, (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na wawakilishi kutoka UNFPA, Benki ya Dunia – Tanzani , watalaam
kutoka Kampuni ya esri inayojishugulisha na kutoa huduma za Mfumo ya Taarifa za
Kijiografia (GIS) pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mara baada ya kumaliza kikao kujadili namna
mfumo wa GIS unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu
mbalimbali nchini.
(Picha zote na Frank
Shija – MAELEZO)
Comments
Post a Comment