SOKO LA SAMAKI KUNDUCHI WABUNI NJIA YA KUWADHIBITI WAVUVI HARAMU.
Na Enles Mbegalo
UONGOZI wa Soko la Samaki Kunduchi, Dar es Salaam
limeunda Kikundi cha Ulinzi Shirikishi
cha Pwani na Baharini (BMU), kwa lengo
la kudhibiti uvumi haramu.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii, mmoja wa
viongozi wa soko hilo, Ramadhani Ali, alisema kikundi hicho cha watu 15
kitafanya doria kwenye fukwe za bahari
kwa masaa 24 ili kuwadhibiti wavuvi hao pamoja na wachafunzi wa mazingira ya
fukwe hizo.
“Ulinzi huu
wa baharini utasaidia sana kuwaokoa baadhi ya samaki ambao wameaza
kupotea kabisa baharini na tutagundua ni samaki wapi hawapatikani kwa sasa na
kipindi cha nyuma walikuwa wanapatikana,”alisema Ali
Pia, alisema
pamoja na serikali kupiga vita uvuvi huo ila inatakiwa kuwasaidia wavuvi
hao vifaa vya kisasa kwaajili ya kuvitumia katika shughuri zao za uvuvi.
Hata hivyo, alisema soko hilo limekuwa likikabiliwa
na changamoto mbalimba ikiwamo usalama mdogo kwa wavuvi kwani wamekuwa wakitishiwa maisha yao na vijana
wasiojishughurisha na shughuri yeyote kwenye soko hilo.
“Kulingana na hali iliyopo sasa kila mtu anatakiwa
kufanya kazi ila vijana wengi wamekuwa wakikimbilia sehemu ya wavuvi na
kutojishughurisha na kazi yeyote,”
Pia alisema soko hilo linakabiriwa na changamoto ya
ukosefu wa vyoo na kupelekea baadhi ya wavuvi wanaoishi kwenye eneo hilo
kujisaidia pembezoni ya fukwe za bahari.
Baadhi ya wavuvi kwenye soko hilo, wakiandaa boti kwaajili ya shughuri za uvuvi.
Mfanyabiashara akiandaa dagaa kwa ajili ya kukaanga na kuuza katika Soko hilo
Kiongozi wa Soko hilo, Ramadhani Ali akionesha Dema ambalo hutumika kwa ajili ya kuvua samaki wakubwa.
Bado wagaangaji wa kitoweo cha samaki wakiwa wanatumia kuni kwa ajili ya shughuli zao kwa wateja.
Baadhi ya vitendea kazi za uvuvi zikiwa zimewekwa kwa ajili ya ukarabati.
Baadhi ya Nyumba wanazoishi wavuvi wakiwa katika shughuli zao za kila siku.
Comments
Post a Comment