Umoja wa Gereji Tegeta waiomba Serikali kuwamilikisha eneo
Na Enles Mbegalo
UMOJA wa Mafundi Gereji Tegeta, jijini Dar es
Salaam,wameiomba serikali kuwamilikisha eneo hilo, ili waweze kufanya kazi kwa
weredi na kuboresha miundombinu ya eneo hilo.
Akizungumza na mwandishi wa habari jana, Mjumbe wa
Miundombinu kwenye gereji hiyo, Mei Hiza alisema changamoto ya miundombinu mibovu ya gereji hiyo sio mizuri na imewafukuzia baadhi ya wateja
wao.
“Kutokuaminishwa eneo hili la magereji limepelekea
sisi kushindwa kufanya kazi kwa weredi na kuboresha miundombinu hii kutokana na
kutokuwa na uhakika na eneo hili ambalo tumewekeza,”alisema Hiza
Aliongeza kuwa “Kama serikali wakituaminisha na
kutumilikisha tutafanya kazi zetu kwa weredi tunashindwa kufanya hivyo kutokana
na migogoro ambayo ilikuwepo kwenye eneo
hili tangu mwaka mwaka 2013,”
Hiza lisema
kutokana na kazi wanazozifanya kwenye gereji hiyo ikiwamo kutengeneza vipuri
vya viwandani, makampuni na watu binafsi wanaiomba serikali iwaangalie kwa
kuwapa kazi mbalimbali ambazo zinatengenezwa kwenye gereji hiyo.
Aidha eneo hilo ambalo liliaza mwaka 2006 likiwa na
mafundi gereji 280 ambapo hadi sasa wamefikia zaidi ya 6000.
Comments
Post a Comment