TAKUKURU IRINGA YAOKOA ZAIDI YA SH. MILIONI 11 ZILIZOKUWA MALIPO HEWA KWENYE ELIMU.
Na Mwandishi wetu, Iringa
TAASISI ya kupambana na rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Iringa
imeokoa jumla ya Sh. Milioni 11,921,800 ambazo zilikuwa ni malipo hewa kutoka
idara ya elimu katika kituo cha Ilula.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii, hivi karibuni ofisini
kwake, Evarist Shija kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru mkoani hapa wakati akitoa taarifa
ya utekelezaji kazi wa Takukuru kwa kipindi cha mwezi Julai 2016 hadi
Machi 2017.
Shija alisema kuwa taasisi hiyo imepokea malalamiko 98 ya
rushwa na 16 kati ya hayo yamefunguliwa majalada ya uchunguzi,malalamiko 15
yanafanyiwa uchunguzi wa awali huku wakifunga malalamiko 67 yaliyoshindwa
kuthibitisha Makosa ya rushwa.
Pia alisema kuwa taasisi hiyo imefikisha mahakamani kesi saba
kwa makosa mbalimbali ya rushwa,na kwa kesi hizo saba ofisi hiyo inafikisha
jumla ya kesi tisa za makosa ya rushwa zinazoendelea mahakamani baada ya kesi
tano kutolewamahakamani kwa kesi mbili kushindwa kuthibitisha makosa ya rushwa
na kesi tatu kuwatia hatiani watuhumiwa.
Alisema katika kesi hizo,
zinahusu watuhumiwa kutoka idara mbalimbali ikiwamo utawala,Afya,Fedha na
ushirika (mtendaji kata uhambingeto,afya wafamasia wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi pamoja na ushirika).
Aliongeza kuwa idara zinazoongoza kwa kulalamikiwa kwa rushwa ni
TAMISEMI ambapo ofisi hiyo imepokea malalamiko 32 kutoka tamisemi,idara za
polisi 13 na elimu 11 na kuongeza kuwa yapo malalamiko kutoka idara za ardhi na
mahakama.
Comments
Post a Comment