WADAU WAMEOMBWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA.
Na Enles Mbegalo
MKURUGENZI wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha
Amani Orphanage, Magreth Mwegalawa,kilichopo
Bagamoyo Mkoa wa Pwani amewaomba wadau mbalimbali kujitoa kwa moyo katika kusaidia watoto hao.
Hayo aliyasema leo mkoani humo wakati wa ufunguzi wa
mabweni mawili ya kulala watoto wa kiume na wakike kwenye kituo hicho.
“Kutoa ni moyo nawaomba wadau mbalimbali wajitoe
kwaajili ya watoto wasiojiweza kwani kufanya hivyo ni kupata dhawabu kwa
Mwenyezi Mungu,”alisema Mwegalawa.
Alisema changamoto zilizopo kwenye kituo hicho ni za
kawaida ikiwamo kukosa chakula, vifaa vya shule hasa kwa kipindi cha miezi ya
kuanza shule na kufungu.
Aliongeza kuwa kituo hicho kilianza na watoto wawili
ambapo hadi sasa wamefikia watoto 38.
Pia alisema kituo hicho kinapokea watoto hao kuanzia
kuzaliwa.
MKURUGENZI wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani Orphanage, Magreth Mwegalawa,akiwa ameongozana na Mchungaji wa Kanisa la Lutherani (KKKT) Usharika wa Boko jijini Dar es Salaam,Hermani Mkini, baada ya kufanya uzinduzi wa mabweni hayo Bagamoyo.
Mchungaji Mkini na Mkurugenzi wa Kituo hicho Magreth akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo leo.
Mchungaji Hermani Mkini akiwa ameketi kabla ya kuaza uzinduzi wa mabweni hayo. (PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG).
Comments
Post a Comment