EVOD, AWAOMBA WANANCHI KUSHIRIKIANA KUTENGENEZA BARABARA YA NGORONGORO.
Na Enles Mbegalo
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Pwani Manispaa ya
Kinondoni Dar es Salaam,Evod Rashid, amewaomba wananchi wa mtaa huo
kushirikiana kutengeneza mitaro ya barabara ya mtaa wa ngorongoro ili kuepuka
usumbufu uliopo kwenye barabara hiyo.
Akizungumza leo na mwandishi wa blog hii, Rashid alisema
barabara hiyo, imekuwa ikitumika na watu wengi ila kwa kipindi hiki cha mvua
imekuwa ikileta usumbufu kutokana na maji kutuwama kwenye barabara hiyo.
“Kila kitu kinahitaji ushirikiano kwa pamoja
tukishirikiana na wananchi wangu tunaweza na nawaomba wasife moyo tushirikiane
kutengeneza mitaro ya kupitisha maji eneo hili ili tuepukane na usumbufu huu
ambao unatokea hasa kwa kipindi hiki cha
mvua,”alisema Rashid
Rashid, alisema kuna wadau wametoa greda kwaajili ya
kutengeneza barabara hiyo, ila kunahitajika fedha nyingi sana kwaajili ya
kuweka mitaro itakayokuwa inapitisha maji na kupeleka baharini.
Mwenyekiti Evod, akiendelea kuonyesha eneo la barabara hiyo linalohitaji ukarabati.
Mfanyabiashara wa mbogamboga akipita katika eneo hilo akisaka wateja.
Baadhi ya wananchi wakipita kwa tabu katika eneo la barabara hiyo. (PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG)....
Comments
Post a Comment