WATANZANIA WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU NA SIO KUTAFUTA NJIA YA MKATO.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATANZANIA, wametakiwa kuwa wavumilivu kwa jambo lolote wanalolifanya na sio kutafuta njia za mkato kufikia malengo yao ambazo zitawafikisha pabaya.
Wito huo umetolewa leo na
Askofu Mkuu wa Dayosisi Kuu ya Dar es
Salaam na Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT), Emmaus
Mwamakula, katika kituo cha Ibada cha Mliman
City Worship Centre (MCC).
“Watanzania tuwe wavumilivu na sio kutafuta
njia za mikato kwenye maisha yetu kwani jambo lolote lile jema hufanywa kwa bidii na sio kutumia njia za
mkato,”alisema na kuongeza
“Tujifunza uvumilivu kama neo la leo lilivyosema, tuogope mambo ya mkato
kwani mambo haya yatatupeleka mahali pasipo pazuri,”
“Mfano katika nchi yetu siku hizi za karibuni Rais Dkt. John Pombe Magufuli
alikabidhiwa Ripoti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali (CAG) na kubaini mambo
mbalimbali ikiwamo baadhi ya watumishi wa umma kugushi vyetu na walifanya haya kwa kupitia njia ya mkato
ili waweze kufika bila kugundua matatizo ya baadaye,”
Aidha,Askofu Mwamakula, alisema wamefungua
kanisa ndani ya Mlimani City kwaajili ya
kuwafikia watu wote bila kuangalia dini zao.
Naye Mtumishi ambaye pia ni Mtaalamu
wa Mionzi ya Tiba kutoka Hospitali ya
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam,
Steven Mkoloma, ambaye pia alihubiri kwenye ibaada hiyo alisema katika
maisha unatakiwa kupambana na haijalishi
upo katika mazingira gani Mungu anamaagano na wewe.
Mkoloma, alisema mipango na bidii
kwenye maisha itakupeleka
kwenye utajiri ila njia za mkato zitakupeleka kwenye umasikini.
Waumini waliohudhulia kwenye idaada hiyo katika kituo cha maombi cha Mlimani City jijini Dar es Salaam leo 30/4/2017 .
Waumini wakiimba nyimbo katika kipindi cha kusifu kilichoongozwa na Mwimbaji wa Injili Tanzania na Muingizaji wa Bongomovie, Silvanus Mumba, akiwa na waimbaji wengine watano wa nyimbo za injili hawapo pichani.
Waumini wakiendelea kumtukuza Mungu katika kipindi cha sifa katika kituo cha Ibada cha Mlimani City.
(PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI.)
Comments
Post a Comment