WAZIRI UMMY: TUSHIRIKIANE KUTOKOMEZA VIFO VYA WAJAWAZITO.
Na Catherine Sungura, W. Afya
WADAU mbalimbali wa sekta ya Afya wametakiwa kufanya juhudi katika kuimarisha afya ya mama mjamzito na mtoto nchini ili kupunguza idadi ya vifo na kujenga taifa imara.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 24 wa Wanasayansi wa ( AGOTA) uliofanyika jijini Dar es salaam .
Waziri ummy amesisitiza kuwa vifo kwa wanawake wenye ujauzito bado ni tatizo sugu nchini, ambalo linahitaji jitihada na nguvu zaidi kupambana nalo ili kutokomeza kabisa tatizo hilo Tanzania.
“Naishukuru taasisi ya AGOTA kwa jitihada inazofanya ikiwemo kuhamasisha uzazi wa mpango,kufanya tafiti mbali mbali, kushauri na utoaji huduma ya Afya kwa mwanamke” alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake, Rais wa AGOTA Prof. Andrea Pembe ametoa pongezi kwa Waziri Ummy kutokana na jitihada anazoendelea kufanya kupitia Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi hiyo.
Comments
Post a Comment