WENYE VIWANDA IRINGA WAIOMBA SERIKALI KUWAPUNGUZIA TOZO ZA KODI.


Na Mwandishi Wetu, Iringa

BAADHI ya wafanya biashara wenye viwanda mkoani Iringa wameiomba serikali kutazama baadhi ya kodi na tozo mbalimbali wanazotozwa ili kuviwezesha viwanda kuzalisha kwa ufanisi ili kuleta ushindani.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wamiliki wenye viwanda mkoani Iringa wakati mwenge wa uhuru ulipopita kuzindua miradi yao ambapo ukiwa kwenye kiwanda cha nyanya cha dabaga katika halmashauri ya wilaya ya kilolo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Petronila Alphonce alimweleza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Hamad Amour kuwa kutokana na tozo hizo baadhi ya bidhaa imekuwa ni ngumu kushindana sokoni.

 Ukiwa kwenye kiwanda cha kuzalisha nguzo za umeme cha Agora kilichopo katika Halmashauri ya Iringa Vijijini mwenge huo ulizindua kiwanda hicho kinachozalisha nguzo za umeme ambapo akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa.

Meneja wa kiwanda hicho Edger Edson alisema pamoja na kuzalisha nguzo zenye ubora kiwanda hicho hakina soko la uhakika jambo linalotishia mustakabali wake.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Hamad Amour alisema ili Tanzania iweze kufikia malengo ya kufikia nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ni vema kila mtanzania kuunga mkono adhma hiyo kwa kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao mbalimbali.

Mwenge huo ukiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ulitembelea shamba la mifugo la kampuni ya Asas Diary na kuzindua miradi ya maendeleo ikiwamo elimu na barabara.

Akizungumza mwakilishi wa kampuni ya Asas Feisal Abri alisema kuwa kampuni hiyo mbali na kujishughulisha na ufugaji wa ng’ombe ,mbuzi na kondoo pia wanajishughulisha na shughuli nyingine za maendeleo ikiwamo ya utunzaji wa mazingira.

Naye Mhandisi wa Manispaa ya Iringa, Mashaka Luhamba, alizungumzia faida ya miradi hiyo na kusema kuwa lengo ni kupunguza msongamano ya matumizi ya barabara ndani ya manispaa hiyo.

 Hata hivyo kiongozi wa mbio za mwenge Amour Amour aliishauri serikali kuwapunguzia wawekezaji wazalendo tozo ya kodi ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa viwanda na kutengeneza ajira kwa vijana.

Aidha ukiwa katika kijiji cha Malinzanga wilaya ya Iringa mwenge huo ulizindua miundombinu ya maji ambao utahudumia wananchi zaidi ya 4,000  huku kiongozi wa mbio hizo akiwaagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuwachukulia hatua kali za kisheria wananchi ambao watabainika kuhujumu miundombinu hiyo ikiwamo kulipa faini ya zaidi ya bomba alilokata.

Michael Chalamila ambaye ni ofisa mtendaji wa kijiji cha Malinzanga alisema kuwa mradi wa ujenzi wa kisima hicho kimegharimu Mil.654 ambapo kati ya hizo  wananchi wamechangia Mil.32 na benki ya dunia ilichangia kupitia mradi wa usafi mazingira sh.612 ili kukamilisha mradi huo.



Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.