MWENYEKITI AIOMBA SERIKALI KUOKOA KAYA 50 ZILIZOZINGILWA NA MAJI.
Maji yakiwa yametuama katika nyumba za wakazi wa eneo la Bunju A Kirungule jijini Dar es Salaam jana, yakiwa na madhara kwa Wananchi waishio hapo kiafya.
Na Enles Mbegalo
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Bunju A Kirungule,
Seif Sitambuli ameiomba serikali kuokoa maisha ya kaya zaidi ya 50 ambazo
nyumba zao zimezingilwa na bwawa la maji
zaidi ya miaka mitatu jijini Dar es Salaam.
Aidha, ameiomba
serikali kutoa maeneo salama kwa wananchi hao ili kuokoa maisha yao
kwa ujumla.
“Ninaiomba serikali iangalie namna ya kuzisaidia kaya
hizi kwani hali iliyopo kwenye maeneo
haya inaweza kuleta maafa zaidi pamoja na kutokea magonjwa ya milipuko,”alisema
Alisema pia athari kubwa inayoweza kujitokea kwa wakazi hao hasa kwa
kipindi hiki hiki cha mvua pia serikali ingeliangalia hilo ili waweze
kuepusha madhara hayo kabla hayajatokea.
“Licha ya serikali kuendelea kutoa misaada mbalimbali lakini tatizo hilo bado ni kubwa
hivyo kupewa kwao viwanja ambavyo viko maeneo salama ingesaidia zaidi,”alisema
Sitambuli
Comments
Post a Comment