ASILIMIA 10 YA WANAUME WAPO HATARINI KUPATA TEZI DUME .
Na Enles Mbegalo
ASILIMIA 10 ya wanaume waliofikia umri wa miaka 40
wapo hatarini kupata ugonjwa wa tezi dume.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii , Mtaramu wa
Madawa na Tiba ( PharmD),
kutoka Hospitali ya Sanitas jijini Dar
Es Salaam, Doctar Sajjad Fazel alisema ugonjwa huo nirahisi kuupata kadri umri
unavyoongezeka.
“Asilimia 10 ya wanaume waliozidi umri wa miaka 40 na waliozidi miaka 60
wanapata tezi dume na kadri umri unavyoongezeka unapata tezi dume,” alisema
na kuongeza
“Tenzi dume ni kiungo kinachopatikana chini ya
kibofu cha mkojo na kinazunguka milija ya mikojo,”
DK. Fazel alisema dalili ya tezi dume ni kukojoa
mara kwa mara, kuchukua muda mrefu ukitaka kukojoa,mkojo kutotoka
kikamilifu,kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Alisema dalili nyingine ni kupata maumivu wakati wa
kufanya tendo la ndoa na ikifikia hatua za mwisho za tezi dume inatoka damu
kwenye mkojo.
“Ugonjwa huu ukitambulika mapema unaweza kutibika
kwa kutumia dawa na kufanyiwa upasuaji,”alisema na kuongeza
“Kama mtu anasaratani ya tezi dume na
haijagundulika inasambaa kwenye viungo vingine vya mwili wake na mwisho wake
anafariki na kama unayo na hujapima ni hatari zaidi kama haijagundulika unaweza
pata saratani ya ini na kibofu cha mkojo,”
Aliwashauri wanaume wote waliozidi miaka 35
wanashauriwa kupima kila baada ya miezi miwili.
Comments
Post a Comment