ASKOFU MWAMAKULA, AKEMEA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII.



Na Enles Mbegalo.

 ASKOFU  Mkuu wa Dayosisi Kuu ya Dar es Salaam na Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT), Emmaus Mwamakula, amewataka vijana kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kwa kutuma vitu sisivyo na manufaa kwa maisha yao.

Hayo aliyasema hivi karibuni,  Mkoani Pwani wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pasaka la Umoja wa Wanafunzi wa Kristo Tanzania(Ukwata).

“Watu hawatumii vizuri mitandao ya kijamii kama mwana Ukwata acha kupost matusi, acha kumuomba mtu urafiki anayetuma picha za ovyo,”alisema Askofu Mwamakula

Alisisitiza kuwa wajifunze kujenga maadili ya watanzania,na sio kutumia mitandao hiyo kwa kueneza chuki kwa watu wengine.

Aidha  aliwataka viongozi wa Ukwata katika kongamano la mwakani kuongeza somo la kuvumiliana.

“Unapokuwa kanisani usikubali kutumika na fujo za siasa  mwanaukwatwa usikubali kabisa kuingia kwenye fujo hizo,”alisema.


Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.