NEMC YAWATOZA FAINI YA SH. MILIONI 20 WAWEKEZAJI WA KILIMO NA MIFUGO.
Na Mwandishi
Wetu, Kilolo
BARAZA la
Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), imewatoza faini ya jumla ya
sh. milioni 20 wawekezaji wawili wa kilimo na ufugaji Wilayani Kilolo kwa
makosa ya kuendesha shughuli zao bila kufanya tathmini ya uharibifu wa
mazingira.
Adhabu hiyo imetolewa na
mwanasheria wa NEMC, David Kongola baada ya kutembelea mashamba ya wawekezaji
hao na kubaini kasoro kubwa za kimazingira na kuhatarisha usalama wa vyanzo vya
maji.
Kongola alisema kuwa
“Sasa adhabu yao hawa sisi tunatoza Mil.10 kwa kila mmoja kwa
kufanya hii shughuli bila ya kuwa na (IAA) Certificate na hiyo ipo wazi kwamba
kifungu no.184 kinasema isizidi Mil.50 na sisi tun asema kwamba Mil.10 na
tutawaletea invoice kwa kuendesha biashara yako bila ya kuwa na cheti cha
tathimini ya mazingira.”alisema Kongola
Adhabu ya NEMC imeyakumba mashamba ya mifugo ya Tomy Dairies
na la Ndoto yaliyopo kwenye kata ya Ihimbo ambapo mwanasheria
wa NEMC alisema sheria lazima zifuatwe kulinda mazingira
Mmiliki wa shamba la Tomy
pia alipewa muda wa wiki moja na kikosi kazi cha kuokoa ikolojia ya Mto Ruaha,
kung’oa migomba iliyopandwa ndani ya eneo la chanzo cha maji cha Mto Ruaha
Mdogo.
Akizungumza Wamoja Ayubu
ambaye ni mjumbe wa kikosi kazi alisema kuwa eneo hilo halitakiwi kupandwa
mazao hayo bali inatakiwa kupandwa miti ya asili ambayo itaendelea kutunza
vyanzo vya maji na hivyo kumtaka kung’oa migomba yote kwa kuhesabu mita 60
kutoka usawa wa mto.
Hata hivyo wamiliki wa
mashamba hayo walikiri mapungufu ingawa walisema kuwa hawakupewa mwongozo
tangu awali.
“ Tumekiri kuwa na
mapungufu hayo na tutajitahidi kuyarekebisha lakini pia sisi hatutaki kufanya
jambo nje ya sheria.”Walisema wamiliki hao
Aidha wamiliki hao
wametakiwa kuvitunza vyanzo vya maji vilivyopo ndani ya maeneo yao kwa faida ya
vizazi vijavyo ambapo David Mginya ambaye ni mjumbe kikosi kazi
alisema kuwa wanatakiwa kujenga miundombinu hiyo kwa lengo la kutunza vyanzo
vya maji.
Comments
Post a Comment