WANANCHI KIJIJI CHA MALIZANGU WAIOMBA SERIKALI KUWABORESHEA MIUNDOMBINU YA SKIMU YA UMWAGILIAJI.
Na Mwandishi Wetu, Iringa
WANANCHI wa Kijiji cha Malizangu Kata ya
Mlowa Wilaya ya Iringa wameiomba serikali kuwajengea miundombinu ya skimu za
umwagiliaji iliwaweze kuboresha kipato na uhakika wa chakula.
Wakizungumza na mwandishi wa blog hii
kwa nyakati tofauti, kijijini hapo walisema kuwa mazao ambayo walitarajia
kuvuna msimu huu yamekauka baada ya mvua kuacha kunyesha.
“kilimo cha kutegemea mvua hakina
uhakika tunaoimba serikali itujengee miundombinu ya skimu za umwagiliaji ili tuweze
kuboresha kipato na uhakika wa chakula,”alisema
Nae, Marian Kamugishi, alisema kata hiyo
mvua zimekuwa za shida,watu wanajuhudi za kulima lakini miundombinu hususani
maji ya umwagiliaji hawana hivyo wanalima kilimo cha kubahatisha.
“Kilimo
hiki hakina maana,tunadhani mkombozi wetu ni pale tunapopata maji ya
umwagiliaji mfano skimu au tukavuna maji ya mvua kupitia mto mlowa na hali ya
uchumi imekuwa ngumu kutokana na mvua kutokunyesha,”alisema
Kamugishi alisema kiujumla kijiji hicho
kinarasilimali kubwa ambayo ni ardhi lakini mwaka huu kumekuwa na janga la
kutokuwa na mvua.
Aliongeza kuwa mvua zimegoma zimeaza
kunyesha mwezi wa pili, wananchi wamelima lakini mazao ndio kama hivyo na maji
bondeni hakuna na kuishauri serikali iwasaidie kujenga banio mlimani kwa lengo
ya kutunza maji kipindi ambacho mvua zimegoma kunyesha.
Kwa upande wake Ofisa Kilimo wa
Kata ya Mlowa, Frank Kasumbi, alisema kuna hekta takriban 6,000 zinazofaa kwa
kilimo cha umwagiliaji lakini changamoto ni kukosekana kwa rasilimali fedha kwa
ajili ya kujenga miundombinu ya kutoa maji ya Mto Ruaha mdogo na kupeleka
kwenye mashamba hayo.
“Bonde hili lina ukame na
mvua ni za shida kitu ambacho kinapelekea wananchi wetu kukosa chakula na kipato
kinazidi kushuka’alisema Kasumbi
Pia alisema changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi
na ukame umeathiri uzalishaji na uapatiakanji wa chakula kwa wananchi wa kijiji
cha Malinzanga kata hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Lulamso
Kadaga alisema wananchi walishabuni mradi wa kutoa maji kutoka Mto Ruaha mdogo
kwaajili ya umwagiliaji lakini mradi umeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu
wa rasilimali fedha.
Kadaga alisema kuwa “Kiujumla
hali ya chakul kwenye kijiji change ni mbaya,kutoakna na mvua kutonyesha kwa
wakati na ziliponyesha zilikatika mapema, mazao ya mahindi, alizeti, ufuta, mtama
na mazao mengine yameshindwa kuvunwa kwa sababu ya ukame, njia pakee ya
kujinusuru ni kuwa na kilimo cha umwagiliaji hasa mfereji.”
Comments
Post a Comment