Rusisye, apiga marufuku wananchi kuendelea kujenga eneo la ngema.
Na Enles Mbegalo
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Kunduchi , Richard
Rusisye amewataka wananchi wa mji mpya eneo la kwa Mkorea kutoendelea kujenga
wala kuishi eneo ambao lipo jirani na ngema ili kuondoka na hali ya kuhatari ya
maisha yao.
Akizungumza na wakazi wa eneo hilo jana baada ya
kwenda kuwapa pole wale walionusurika na kifo wakati ngema la eneo hilo
lilipodondokea nyumba zao usiku.
“Ujenzi sambamba na eneo hili haturuhusu na tutakuja
kuweka alama ya x na baadhi ya
nyumba na watu watalazimika kubomoa
nyumba zao na kuhama eneo hili kwani ni hatarishi kwa maisha yao,”alisema
Rusisye
Aliongeza kuwa“miaka mitatu iliyopita lilidondoka ngema
na kufukia watu wawili na mwaka jana nilikuja hapa nikawazuia msijenge eneo hili kwani si salama kwa maisha
yenu,”
Alisema uvumilivu umefika mwisho kwani yanapotokea
majanga wanapoteza nguvu kazi ya taifa na marufuku mtu yeyote kuendelea
kuchimba kokoto hapo.
Naye, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Kawe
OCD, John Malulu, alisema wao kama viongozi watarazimika kuwaondoa watu
waliojenga nyumba zao jirani na ngema hilo ili kuokoa maisha yao kwani maeneo
hayo ni hatarishi.
Malulu, alisema
mfumo wa serikali unaaza na ngazi ya
mtaa ni lazima watu wachukue tahadhari.
Alitoa onyo kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo
kutogusa ngema hilo lililodondoka kwa
kuchimba kokoto na atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua.
“Msiguse hili
ngema lililodondoka kwa kuchukua mawe
haya na tutaweka ulinzi hapa atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria,”
Naye, Renatha Kaijage, ambaye ni mmoja wa wahanga wa
nyumba zilizondokewa na ngema hilo, alisema ngema hilo lilidondoka majira ya
saa sita usiku ila yeye hakuwemo eneo
hilo.
“ Majira ya saa tano usiku dada aliniita niliporudi
nilikuta ngema hili limedondokea nyumba ninayoishi, namshukuru Mwenyenzi Mungu
maana ningekuwepo ningekufa,’
Comments
Post a Comment