SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.
Na Mwandishi Wetu, Mafinga. SERIKALI imerejesha kambi tano za JKT zilizokuwa zimesitishwa mafunzo ya jeshi hilo ili kuongezea uwezo zaidi wa kuchukua vijana na kuwajengea uwezo wa kuwa hodari,watiifu na waaminifu katika kambi zake. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii JKT Taifa Luten kanal Anchilla Kagombola kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo meja jenarali Michael Isamuyo kwenye hitimisho la mafunzo ya vijana wa kujitolea (JKT) kikosi 841 KJ mafinga operation. Kambi zilizorejeshwa ni kambi 826 KJ Mpwapwa Dodoma, kambi 839 KJ Makuyuni Arusha, kambi ya 845 Itaka Songwe,846 Luha Rukwa na kambi 847 Milundokwa Rukwa na kati ya kambi hizo kambi la Makuyuni Arusha tayari wa meshaanza kuchukua vijana na wanaendelea na mafunzo. Kagombola alisema ni Imani ya Mkuu wa JKT kuwa serikali inazidi kutoa mchango wa hali na mali ili kuzidi kuboresha miundombinu ...
Na Mimi nikitka kujifunza na fanyaje
ReplyDelete