BUNDU, MBUNIFI WA SIMU YA "KIFUU"AMBAYE HAKUNUFAIKA NA KAZI YAKE.

Bundu, akiwa na vitu vingine alivyobunia ambavyo ni kobe wakieletroni pamoja na simu yenye umbo la ndege mnyama.
Peter Akaro.

ALLY Bundu ni kijana ambaye anajishughulisha na ubunifu kwa kipindi kirefu, ingawa kwasasa amekata tamaa kutokana na mambo aliyokutana nayo katika kazi za ubunifu.

Kabla ya hayo, Bundu amebuni Simu ya Mezani ya Kifuu cha Nazi, hii simu ni kwaajili ya kudhibiti upotevu wa simu kadi (hasa kwa kipindi cha nyuma ambapo kulikuwa hakuna huduma ya kurejesha simu kadi).

Simu hii ya kifuu inaweza kutumikia wakati haina simukadi (laini), pengine mtumiji ameificha sehemu isiyoweza kuonekana na wezi, na mtumiaji anaweza kuwasiliana bila matatizo yoyote ya kimtandao.

Vitu vilivyo unda simu. 
 
Anasema kitu cha kwanza ni kifuu cha nazi kama kava la nje, kandambili kwaajili vibonyezeo (baton), wayaza ‘transformer’, kioo (display) cha simu ya Motorola, kadi ya deki ya runinga (simsung) kwaajili ya kunukuu mtandao (network).

“Kadi ni kwaajili ya kuhifadhi kumbukumbu, kwa mfano umeme unapo katika na baadae kurudi, picha (video) uliyo kuwa unaitaza inaendelea pale pale ulipoishia, na hivyo hivyo ukiingiza mtandao inahifadhi,” anasema na kuendelea.

“Kitu kingine ni ‘power system (power IC)’na ‘network system (network IC)’ ya simu, kisha ni Kaunda saketi kama ya simu ya kawaida, ambapo ‘power system’inaingiza taarifa kwenye ile kadi ya deki na kupeleka kwenye ‘network system’,”anasema.

Anaongeza  kuwa vitu vingine vilivyo unda simu hii ya kifuu ni pamoja na ngozi ya ng’ombe, betri ya simu, mbao, spika ya kawaida, majani ya makuti ya mnazi na mchanga.

Namna inavyo fanya kazi

“Ufanyaji kazi wake unaweka simu kadi ya mtandao wowote kisha unaiweka…pale inapo isoma ‘network’ wewe unaweza ukaitoa simu kadi na bado mawasiliano ukawanayo,” anasema.

“kitu ambacho kinafanya uendelee kupata mawasiliano licha  ya kutoa simu kadi ni ile deki ya runinga inayotunza kumbukumbu kama nilivyoeleza hapo awali,” anasema.

Anasema, unaweza kuweka vocha wakati simu kadi haipo kwenye simu na kupiga lakini kwa wakati anaunda simu hiyo (mwaka 2009) mitandao ya simu bado ilikuwa haijaanza kutoa huduma ya kuunga vifurushi.

“Na simu kadi unaweza kuiacha sehemu yoyote wewe ukaondoka na simu na ukaendelea kupata mawasiliano, ila kuna kitu cha muhimu cha kukumbuka,” anasema na kuendelea.

“Kama  umeacha simu kadi nyumbani au upo mbali na simu kadi, simu usije ukaizima kwa sababu itahitaji simu kadi ili iweze kusoma mtandao (network) kwanza na kisha kuibakiza kwenye ile deki ya runinga,” anasema
Simu ya Mezani iliyoundwa kwa kifuu cha nazi.
...........
Wazo la kubuni simu.

Anasema, wazo lilimjia mwaka 2008 baada ya kuona maeneo ya Ubungo na Manzese wizi wa simu za mkononi umeshamiri kwa kiasi kikubwa.

“Ni baada ya kuona hamna huduma ya kurejesha simu kadi (renew), na kwa wakati uleni bora ukapoteza simu au kuibiwa kuliko simu kadi,” anasema na kuongeza.

“Hivyo mimi nikaja na hili wazo ili kuondoa hilo tatizo japo kuwa hakuna aliyetambua uwezo wangu,” anasema.

Anaongeza, hapo awali alitengeneza simu ya kifuu ya mkononi lakini kutokana na mazingira na wasiwasi kuwa watu kutomuelewa, ndipo akatengeneza simu ya kifuu ya mezani.

Safari  yake ya ubunifu.

Anasema msanii wa bongo fleva Hamad Ally‘Madee’ ndie mtu wa kwanza kuona ubunifu wake kwa kuwa walikuwa wanafahamiana tangu utotoni alipokuwa akiishi Manzese.

“Madee alipoona hii simu ya kifuu alivutiwa nayo na kuniunganisha  kwa mwandishi wa gazeti la Mtanzania Kambi Mbwana ambaye nilifanyanae mahojiano kuhusiana na hii simu na ile kazi akaitoa,” anasema na kuongeza.

“Baada ya hapo watu wengi wakaanza kunitafuta kikiwemo kituo cha runinga cha East Africa Television (EATV) ambacho nilifanya nao kipindi cha Uswazi, na hapo watu wengi wakazidi kunifahamu zaidi,” anasema.

Anasema haikuchukua muda akapigiwa simu kuwa anahitajika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo kwa kipindi hicho alikuwa William Lukuvi.

“Nilipofika kwa Lukuvi akachukua hii simu akaweka simu kadi yake (Celtel) na kuwasha, kisha akaitoa na kupiga, kweli simu ikaita…basi akafurahi,” anasema na kuongeza.

“Lukuvi akaniambia yeye amepigiwa simu na Rais Kikwete kuwa mimi nichague shule yoyote ambayo nataka kusoma na fedha italipwa kutokaTaasisiyaWanawake na Maendeleo (WAMA) ya Mama Salma Kikwete, basi ni katoka pale na gari la Mkuu wa Mkoa hadi Veta Chang’ombe ambapo mimi nilichagua,” anasema.

Anaongeza alipofika Veta walimu, walifurahi kuona ubunifu wake, kisha alielezwa anatakiwa kusoma kozi ya miezi mitatu ambayo ada yake ni sh. 3,400,000 na mchakato wamalipo pamoja na kujiunga ukaanza.

“Kesho yake nikaelekea Wama nikiwa na simu yangu, na pale nikakabidhiwa kwa Ofisa ambaye nilielezwa atakua anasimamia masuala yangu ya shule na yeye atakuwa anayapeleka kwa Mama Salma” anasema.

Kutotimia kwa ndoto zake.

Anasema kwa bahati mbaya pale Wama hakupata masaada wowote wa kwenda shule kama alivyoelezwa hapo awali.

“Ikawa kila siku nafuatilia hadi ikawa kama ni deni lakini nikawa narudi patupu, baadae nikaamua kuachana nao…kama riziki ni yangu itarudi tu,” anasema.

“Basi ni kaamua niachane na mambo ya ubunifu kwa sababu Tanzania mambo ya ubunifu bado hayajatambulikaa sana, ndipo nikamua kujikita zaidi katika ufundi wa simu, redio, runinga, computer nakufungamadishi (vingamuzi),” anasema.

Mwandishi: Peter Akaro
Contact: 0755 299596

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.