OFISA MISITU KILOLO,ASHINDWA KUDHIBITI VYANZO VYA MAJI.
Na Mwandishi
Wetu, Kilolo
OFISA Misitu wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kilolo mkoani Iringa ,Eugen Mwilafi, amejikuta katika wakati mgumu baada ya
kushindwa kutoa ufafanuzi wa kutosha kwa nini halmashuri hiyo imeshindwa
kudhibiti kilimo kwenye vyanzo vya maji.
Hali
hiyo imetokana na kukithiri kwa kilimo cha mabondeni maarufu kama vinyungu
kando kando ya mito ya Mtitu na Lukosi inayotiririsha maji kwenye mito ya Ruaha
Mdogo na Mkubwa.
Ongezeko
la kilimo cha vinyungu wilayani kilolo limebainishwa pia na viongozi wa
wilaya hiyo mbele ya wajumbe wa kikosi kazi cha kuokoa ikolojia ya mto Ruaha
Mkuu iliyoundwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu hivi karibuni wakati akiwa
mkoani Iringa.
Akizungumza
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah, alisema inatakiwa wanaolima kwenye
vinyungu kutolewa kwenye eneo hilo na kupelekwa kwenye ufugaji wa samaki au
watafute maeneo mengine ambayo yanafaa kwa shughuli za uzalishaji mali.
Wajumbe
wa kikosi hicho walishuhudia mahindi yakiwa katikati ya vyanzo vya maji katika
vijiji vya Idegenda, Madege na Kidabaga.
Hata
hivyo ofisa Misitu huyo aliwekwa kitimoto na kikosi kazi “Sasa wewe hata kama
wanafanya wengine wapo chini ya usimamizi wako na anayevuruga unaweza
kumchukulia hatua za kisheria.”walisema wakati wakimweka kitimoto ofisa huyo
Hata
hivyo hali ilikuwa ya kuridhisha katika chanzo cha mto Lukosi kwa kuwa kuna
usimamizi mzuri wa viongozi wa kijiji cha Idete lakini wananchi walitaka zoezi
la kuzuia vinyungu liwe la wilaya nzima.
“Tupo
makini katika kutunza mazingira lakini hatujafahamu vijiji vya jirani kwamba
hili linakuwaje alipoulizwa kuhusu sheria ya yoyote wanayoisimamia alisema kuwa
sheria ipo na inasema kwamba mtu akichoma moto wanamtoza faini y ash.50,000
hadi 100,000.”walisema wananchi hao.
Aidha
kikosi kazi hicho kilimtaka ofisa wa Misitu wilaya kusimamia sheria za
mazingira na kuomba ushauri pale anapokwama ili kunusuru vyanzo vya maji.
Comments
Post a Comment