SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.
Na Mwandishi
Wetu, Mafinga.
SERIKALI imerejesha kambi tano za JKT
zilizokuwa zimesitishwa mafunzo ya jeshi hilo
ili kuongezea uwezo zaidi wa kuchukua vijana na kuwajengea uwezo wa kuwa
hodari,watiifu na waaminifu katika kambi zake.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa
Ustawi wa Jamii JKT Taifa Luten kanal Anchilla Kagombola kwa
niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo meja jenarali Michael Isamuyo
kwenye hitimisho la mafunzo ya vijana wa kujitolea (JKT) kikosi 841
KJ mafinga operation.
Kambi zilizorejeshwa ni kambi
826 KJ Mpwapwa Dodoma, kambi 839 KJ Makuyuni Arusha, kambi ya 845 Itaka
Songwe,846 Luha Rukwa na kambi 847 Milundokwa Rukwa na kati ya kambi hizo kambi
la Makuyuni Arusha tayari wameshaanza kuchukua vijana na
wanaendelea na mafunzo.
Kagombola alisema ni Imani ya Mkuu wa JKT kuwa serikali inazidi
kutoa mchango wa hali na mali ili kuzidi kuboresha miundombinu ya vikosi vya
JKT na hatimaye kuwawezesha vijana wengi wa Tanzania wenye sifa za kujiunga na
mafunzo hayo kwa kujitolea na pia kuchukua vijana wengi kwa mujibu wa sheria wanaomaliza
kidato cha sita.
“Ninyi vijana mnaohitimu leo hii,
mafunzo haya yasitumike kupiga raia wema ninyi ni sehemu ya jamii ni watoto wa
wakulima na wafanyakazi wanaohitaji ulinzi kutokana kwenu shirikianeni na
mamlaka husika kuwafichua waovu wasaliti na wale wote wasiotakia Nchi yetu amani
na utulivu tuliyonayo.”alisema Kagombola.
Awali akisoma risala ya wahitimu hao
Diana Jason Ngaiza alisema, wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wakufunzi
wa kada ya juu, ukosefu wa vifaa vya kuendeshea mafunzo hali ambayo imepelekea
mafunzo kufanyika kwa shida.
Naye Mkuu wa Kikosi hicho, Luten Kanal Hamis Mahiga alisema kwa kipindi kifupi walichokaa kikosini hapo wameweza kuwaachia vitu mbalimbali vya maendeleo ikiwamo mashine ya kusaga na kukoboa,bwala la samaki na jenereta vitu ambavyo miaka ya nyuma vilikuwa havipo.
Mahiga alisema lengo la kuwapa nyenzo tatu kwenye kiapo chao ikiwamo uadilifu,utii na uhodari ni kuwatengezea uwezo wa kwenda kubadilisha changamoto zilizopo kwenye jamii kuwa fursa pindi wanapohitimu mafunzo yao.
Kwa upande wake mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William alisema baadhi yao watapata nafasi ya idara mbalimbali za serikali katika utumishi wa umma huku akiwataka watumie nafasi hizo kwa kuzienzi kama tunu ili waweze kufanya kazi hizo kwa nidhamu ya hali ya juu.
Pia, William aliwaomba vijana ambao watarudi uraiani washiriki na wananchi wengine katika kuzalisha mali ikiwamo kilimo,ufugaji,viwanda,ujasirimali pamoja na kulinda taifa ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi katika taifa hili.
Comments
Post a Comment