UPONYAJI WAZIDI KUTENDEKA KATIKA KITUO CHA IBADA CHA MLIMANI CITY.

Miongoni mwa watu waliofika MCC kuombewa jana ni watu wawili ambao walikuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwamo maumivu ya mgongo, ganzi ya mwili nk.

Aidha watu hao walifika MCC baada ya kusikia taarifa za ibada kupitia mtandao, pia walifurahi kuondoka kituoni hapo baada ya kufunguliwa.

Baada ya kufunguliwa na kuponywa watu hao waliondoka  kituo hapo wakiwa na furaha na amani mionyoni mwao.

Hata hivyo muumini mmoja ambaye alienda pale akiwa akisumbuliwa na kichwa na macho, alishuhudia  kuwa baada ya kuombewa alipona tatizo hilo, hadi sasa hatumii  tena miwani.
MKUU wa Kanisa la Morovian la Uamsho Tanzania  (KMUT), Mhashamu Askofu Emmaus Mwamakula, akihubiri katika ibada ya jana katika kituo cha  Mlimani City Worship Centre (MCC) katika ukumbi wa sinema uliopo ndani ya jengo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mhashamu Askofu, Mwamakula akisalimiana na Shemasi Mlei Joseph Samson, baada ya kumtambulisha kuwa  Shemasi Mle katika kituo ch MCC.
Mhashamu Askofu Mwamakula, akiwa na Mashemasi Walei wa kituo cha MCC, wa  pili kulia kutoka kwa Askofu ni Shemasi Mlei Irene Mbalwa, anayefuata kutoka kwa Mbalwa ni Shemasi Mlei  Neema Mwaipopo na wa Mwisho kushoto ni Shemasi Mlei Joseph Samson.
Waumini wakiendelea kumtukuza Mungu katika kipindi cha sifa jana, katika kituo cha MCC.
 Waumini wakishiriki kipindi cha kusifu na kuabudu jana.
Martha Patrick, kushoto  akiongoza kipindi cha sifa leo akiwa na Mwimbaji wa Muziki wa Nyimbo za Injili Nchini, Christina Seme kulia.
Mwimbaji wa Muziki wa  Nyimbo za Injili Nchini, Richard Mmari aliyetangazwa rasmi jana kuwa Shemasi Mteule wa MCC akiongoza kipindi cha sifa katika ibada ya jana, Shemasi Mlei Mteule anatarajiwa kubarikiwa rasmi baadaye kuwa Shemasi Mlei wa MCC.
 Waumini wakiendelea kusifu, katika kituo cha ibada cha MCC jana .
Kipindi cha sifa kikiendelea jana katika kituo cha ibada MCC, ambapo ibada ya maombezi hufanyika kila siku ya jumapili katika ndani ya ukumbi wa sinema uliopo ndani ya jengo la Mlimani City.
 Mwimbaji wa Muziki wa Nyimbo za Injili Nchini, Seme akiendelea kuongoza kipindi cha kusifu na kuabudu jana.

Mbali na MCC ibada za sifa, Neno  na maombi ya uponyaji na kufunguliwa hufanyika muda huo huo katika vituo vya Kanisa la Morovian la Uamsho Tanzania Ushirika wa Mbweni eneo la Boko Magengeni na Kanisa la Morovian la Uamsho Tanzania Ushirika wa Golani eneo la Kimara Suka jirani na Kanisa Katoliki kule Golani na ibada katika vituo vyote  ni saa 8:00 hadi 11:00 asubuhi kwa mawasiliano zaidi piga simu 0767086884.


Comments

  1. Amen kwa kazi ya MUNGU. Mhasham Askofu Mwamakula MUNNGU aendelee kukubariki na kukutia nguvu katika kazi yake ili injili isonge mbele.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.