MBUNGE CHUMI AKABIDHI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA.
Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini (CCM) Cosato Chumi , kushoto akikabidhi gari la kubebea wagonjwa ambulance nyingine mpya yenye thamani ya sh Milioni 150 kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mafinga Mji Charles Makoga, kulia ambalo litatumika katika kituo cha afya cha Ihongole kilichopo kwenye jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi akizungumza na wananchi pamoja na uongozi wa Halmashauri wakati akikabidhi gari la kubebea wagonjwa kwenye kituo cha afya cha Ihongole kilichopo wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi, kushoto akikabidhi vitanda 35 dabo deka vyenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 6.5 katika Shule ya Sekondari Isalavanu, iliyopo kwenye Jimbo hilo ambavyo vitatumika kwenye bweni la wasichana ambapo Mbunge huyo ameridhia kutoa mara baada ya kutembelea shule hiyo na kuwakuta wanafunzi wakike wakiunganisha viti ili viwe vitanda, anayepokea ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mafinga Mji Charles Makoga, kulia.
Hivi ni vitanda ambavyo Mbunge Chumi amevikabidhi katika Shule ya Sekondari Isalavanu.
PICHA ZOTE NA MPIGA PICHA WETU MAFINGA.
Comments
Post a Comment