WAUMINI WAZIDI KUTOA SHUHUDA ZA UPONYAJI NDANI YA MLIMANI CITY.

Askofu Mkuu wa Dayosisi Kuu ya Dar es Salaam na  Mkuu wa Kanisa la Uamsho la Morovian la  Tanzania (KMUT), Mhashamu Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula akimsikiliza Petra alipokuwa akitoa ushuhuda Kanisani leo baada ya kuponywa uziwi, Petra ambaye sasa ni Mwanafunzi wa Kidato cha Pili Katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa, alieleza kuwa alianza kutosikia vizuri tangu  akiwa Darasa la nne na alieleza kuwa baada ya kuombewa anasikia bila shida, pia maumivu ya mgongo, kichwa na sikio yamekoma.

Mhashamu Askofu Emmaus Mwamakula pamoja na jopo la Mashemasi Walei wakimuombea baraka za Mungu binti aitwaye Petra aliyeponywa na kufunguliwa kutokana na pepo la uziwi, ibada hiyo ilifanyika leo 25 Juni 2017 katika kituo cha ibada cha Mlimani City Worship Centre (MCC).

Mhashamu Askofu Emmaus Mwamakula pamoja na jopo la Mashemasi Walei wakiiweka wakfu mimbari inayohamishika (Movable Pulpit), iliyotolewa kama sadaka na familia ya Dkt. Charles Sokile (PhD) kwaajili ya kituo cha Mlimani City Worship Centre.

Mhashamu Askofu Emmaus Mwamakula akiwa na Grace Mgumba ambaye ni mama wa Petra, binti aliyeponywa na kufunguliwa kutoka katika tatizo la uziwi, Grace alishuhudia kuwa binti yake huyo alipopimwa Hospitalini aligundulika kuwa mshipa mmoja wa fahamu ulikuwa umeharibika hivyo akaamua kumpeleka binti yake katika shule maalum inayopokea watoto wenye uziwi ambapo mtoto wake alijifunza hata lugha ya viziwi, Grace alionyesha kumshukuru Mungu kuona binti yake sasa anaweza kusikia bila shida.

Dkt. Charles Sokile (PhD) akihubiri MCC kwa lugha ya Kiingereza huku mke wake Rosemary Bagoka -Sokile akitafsiri kwa lugha ya Kiswahili.

Mhashamu Askofu Emmaus Mwamakula, akiwabariki watoto waliofika kuabudu MCC leo.

 Mhashamu Askofu Emmaus Mwamakula, pamoja na Dkt. Charles Sokile wakimuombea mmoja wa waumini waliokuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali yaliyokuwa yanasababishwa na nguvu za giza.

Mwinjilisti Mbogo, akiongoza kipindi cha kusifu na kuabudu leo katika kituo cha ibada cha MCC.

Waumini wakiendelea kusifu na kuabudu leo katika kituo cha MCC.

Mhashamu Askofu Emmaus Mwamakula pamoja na jopo la Mashemasi Walei wakimuombea baraka Dkt. Charles Sokile pamoja na familia yake baada ya kutoa sadaka ya mimbari itakayotumika katika kituo cha MCC.

 Waumini wakiwa kwenye maombi leo katika kituo cha MCC.

Waumini wakiendelea kumwimbia Mungu leo katika kituo cha ibada cha MCC.

Waumini wakiendelea kumtukuza Mungu leo katika kituo hicho cha  cha ibada.

Ibada za sifa neno na maombi ya uponyaji na kufunguliwa kutoka katika nguvu za giza hufanyika kila Jumapili pale Mlimani Worship Centre (MCC) katika Ukumbi wa Sinema uliopo ndani ya Mlimani City Mall jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2:00 hadi 5:00 asubuhi na hakuna kiingilio maombi hufanywa bure pasipo malipo kwa mawasiliano zaidi piga simu 0767086884.

Kituo cha Mlimani City Worship Center (MCC) ni Tawi la Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT).

Matukio ya maombezi ya ibada hii hutolewa na  (MAISHA NI HABARI BLOG).


Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.