KUFUNGULIWA KATIKA SHIDA MBALIMBALI KULIVYO TEKA KITUO CHA IBADA CHA MCC.

Mkuu wa Kanisa la Morovian la Uamsho Tanzania (KMUT), Mhashamu Askofu Emmaus Mwamakula, pamoja na watumishi wa Mungu wakimuombea  dada huyo jana katika kituo cha  ibada cha Mlimani City Worship Centre (MCC), katika ukumbi wa sinema uliopo ndani ya jengo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Waumini waliohudhuria ibada ya jana katika kituo cha MCC wakiwa katika maombi, wakati watumishi wa Mungu wakiendelea kutoa huduma ya maombezi kwa watu wenye matatizo  mbalimbali ikiwamo magonjwa.
Waumini wakiendelea na maombi jana katika kituo cha ibada cha MCC, katika ibada ya maombezi na kufunguliwa katika shida mbalimbali ambayo hufanyika kila siku ya Jumapili kuanzia saa 2:00 hadi 5:00 asubuhi.
 Dkt. Charles Sokile (PhD) aliyevaa suti  pamoja na Mashemasi Walei wa MCC, wakishiriki kumuombea mtoto aliyelipuka mapepo wakati wa maombezi katika ibada ya jana MCC, mtoto huyo alikuwa akisumbuliwa na pepo la pumu, alisafirishwa na wazazi wake wanaoishi Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuombewa katika kituo cha ibada cha MCC, baada ya kuona  akiteseka  bila kupona, baada ya maombi mtoto huyo alionekana mwenye furaha baada ya pepo kumwachia.
Mashemasi walei wa kituo cha MCC wakiongoza kipindi cha Sifa jana.
Waumini wakiendelea kusifu na kuabudu  katika kituo cha ibada cha  MCC,  na ibada hiyo  hufanyika kila siku ya jumapili katika ukumbi wa sinema uliopo  ndani ya jengo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Waumini wakiendelea kusifu na kuabudu katika ibada ya jana katika kituo cha MCC.
Mkuu wa Kanisa la (KMUT), Mhashamu Askofu Mwamakula, akiwatambulisha Dkt. Charles Sokile (PhD) pamoja na mke wake Rosemary Bagoka Sokile mbele ya waumini katika kituo cha MCC, Dkt. Sokile ndiye aliyehubiri katika ibada ya jana na somo lilitoka katika kitabu cha Zaburi 105:17.
Mkuu wa Kanisa la (KMUT), Mhashamu Askofu Mwamakula, akiwabariki watoto waliofika katika kituo cha ibada cha MCC, baada ya kuwabariki aliwaruhusu watoto wote kwenda kuanza ibada yao.
Mashemasi Walei wa kituo cha MCC wakiendelea kuongoza kipindi cha kusifu na kuabudu.
Mkuu wa Kanisa la (KMUT), Mhashamu Askofu  Mwamakula, akimuongoza kula kiapo cha utii na uaminifu Shemasi Mlei Richard Mmari katika ibada ya jana  MCC.
Mkuu wa Kanisa la (KMUT), Mhashamu Askofu Mwamakula, akimuongoza Shemasi Mlei Mteule Mmari katika kiapo cha utii na uaminifu kabla ya kubarikiwa kuingia kwenye daraja la Shemasi Mlei, nyuma yake  ni Mashemasi Walei pamoja na Mzee Kiongozi Dkt. Gloria Manyangu (MD) aliyevaa nguo za bluu pamoja na Mashemasi Walei wa  MCC.
Mkuu wa Kanisa la  (KMUT), Mhashamu Askofu  Mwamakula, na Mashemasi Walei wa  MCC wakimuwekea mikono Mmari, wakati alipokuwa akibarikiwa kuwa Shemasi Mlei jana.
Shemasi Mlei wa MCC Mmari akipeana mikono na Mashemasi Walei wa MCC baada ya kuapishwa na kisha kubarikiwa kuingia katika daraja hilo jana.
Waumini wakiendelea kusifu na kuabudu leo katika kituo cha MCC.

Watu wote wenye shida mbalimbali wanatiwa moyo kuja kuombewa katika kituo cha MCC kila siku ya Jumapili kuanzia saa 2:00 hadi 5:00 asubuhi, na hakuna malipo yanayohitajika kwa mawasiliano zaidi piga simu 0767086884.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.