DIWANI ASHIRIKI USAFI KABLA YA KUFANYA UZINDUZI WA KAMPENI YA WEZESHA MAMA NA MTOTO MPYA KUNDUCHI.
Diwani Michael Urio, akifyeka majani nje ya Zahanati ya Mtongani, kabla ya kuzindua wa Kampeni ya Wezesha Mama na Mtoto Mpya Kunduchi leo jijini Dar es Salaam yenye lengo la kujenga wodi ya akina mama pamoja na chumba cha upasuaji katika Zahanati hiyo na Ununio Kata ya Kunduchi.
Diwani Urio akiendelea kufanya usafi pamoja na vijana wa joggingi Kata ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Diwani Urio akiendelea kufanya usafi na vijana wa joggingi Kata ya Kunduchi katika uzinduzi wa kampeni hiyo leo, iliyofanyika katika Zahanati ya Mtongani.
Hawa ni baadhi ya vijana wa joggingi kutoka Kata ya Kunduchi walioshiriki kufanya usafi katika Zahanati ya Mtongani kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo.
Diwani Urio, kushoto akisalimiana na mmoja wa wageni waalikwa Luteni Baraka Myala waKunduchi Transt Camp (KTC), kulia waliofika kwaajili ya kushiriki usafi na uzinduzi wa kampeni hiyo leo, katikati ni Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Kinondoni,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Kinondoni, Florence Masunga .
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Kinondoni,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Kinondoni, Florence Masunga akishiriki usafi na baadhi ya vijana wa joggingi walioshiriki kufanya usafi katika Zahanati ya Mtongani kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo leo.
Vijana wakiendelea kufanya usafi nje ya Zahanati ya Mtongani leo.
PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG.
Comments
Post a Comment