DIWANI URIO AZINDUA KAMPENI MPYA YA WEZESHA MAMA NA MTOTO MPYA WA KUNDUCHI IKIWA NI MOJA YA AHADI ZAKE.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Diwani wa Kata ya Kunduchi, Michael Urio amezindua
kampeni ya Wezesha Mama na Mtoto Mpya wa
Kunduchi kwaajili ya ujenzi wa wodi ya akina mama pamoja na chumba za
upasuaji katika zahanati ya Mtongani na Ununio ili kupunguza vifo vya mama na
mtoto.
Aidha Kampeni hiyo iliambatana na ufanyaji wa usafi katika Zahanati ya Mtongani ili kuboresha
mazingira ya zahanati hiyo.
Akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo leo
jijini Dar es Salaam, Urio alisema kampeni hiyo ni moja ya ahadi ambazo
aliahidi wakati wa uchaguzi ambapo vipaumbele vyake vilikuwa sita ikiwamo kuboreshaji mazingira ya Afya, elimu.
Vipaumbele vingine mazingira ambapo hadi sasa Kata
hiyo inakitaru cha miti zaidi ya 6000, kuboresha uchumi wa wananchi, Soko la samaki
la Kunduchi , sanaa na michezo na Utawala bora.
“Uzindunzi wa Kampeni hii ya Wezesha Mama na Mtoto
Mpya wa Kunduchi ni moja ya utekelezaji wa ahadi ambazo niliahidi wakati wa uchaguzi ,”alisema
Diwani Urio alisema uzinduzi wa kampeni hiyo
utaendana na uboreshaji wa viwanja vya
wazi vya mipira, Mashindano ya mpira Urio
Cup, upandaji wa miti, riadha pamoja Msonge Mara Soni ambayo itazinduliwa siku za
karibuni.
Aliwaomba
wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia ili aweze kutekeleza
ujenzi wa chumba cha upasuaji katika
zahanati ya Mtongani na Ununio.
“Kupitia Kampeni hii nitahakikisha nasimamia vizuri
na wadau wa makampuni, Taasisi za kifedha tunaomba mtupokee vizuri tutakapo
kuja kwaajili ya kuwaomba ili tuweze
kufikia lengo la kupata sh. milioni 300 kwaajili ya kufikia lengo letu,”alisema
Alisema kupitia Halimashauri ya Manispaa ya
Kinondoni wameweza kupatiwa zaidi ya sh.milioni 3 kwaajili ya kuboresha
Zahanati ya Tegeta, sh. milioni 100 kwaajili ya kuboresha Soko la Tegeta Nyuki
na sh. milioni 150 kwaajili ya kuboresha soko la samaki Kunduchi.
Naye, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Festo
Dugange alisema lengo la Serikali kuboresha ni kuboresha huduma ya mama mjamzito
na mtoto chini ya miaka mitano ili kupunguza idadi ya vifo ambavyo vimekuwa
vikitokea.
Katika uzinduzi wa Kampeni hiyo wananchi na wageni
waalikwa waliohudhuria wamechangia zaidi ya sh. Milioni 4 na mifuko ya saruji
50.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu, kulia akimpongeza Diwani Urio kwa kuzindua Kampeni hiyo itakayosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Kinondoni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Kinondoni, Florence Masunga, kulia akitoa ahadi yake ya kuchangia sh. 500,000 ili kuunga mkono juhudi za kampeni hiyo, kushoto ni Diwani Urio.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Festo Dugange, kulia akizungumzia juu ya jitihada za Serikali za kukabiliana na vifo vya mama na mtoto na ameahidi kuchangia mifuko ya sumenti 15 kwaajili ya Kampeni hiyo kushoto ni Diwani Urio.
Diwani Urio, kushoto akiwa kwenye mazungumzo na baadhi ya wageni waalikwa kabla ya uzinduzi wa Kampeni hiyo leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Meja Msaki kutoka chuo cha NDC,na kulia ni Luteni Baraka Myala kutoka Kunduchi Transt Camp (KTC).
Diwani Urio, kushoto akiwa na picha ya pamoja na wageni waliohudhuria uzinduzi huo, wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwe Pande Suzan Massawe.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kilongawima Kata ya Kunduchi,John Rugakila akitoa ahadi ya kuchangia mifuko 10 ya sumenti baada ya kukaribishwa na mwenyeji wake Diwani Urio katika uzinduzi wa Kampeni hiyo leo.
Diwani Urio akikabishia fedha taslimu sh. 200,000 kutoka kwa Meja Margreth Msaki kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDS) kwaajili ya kuchangia juhudi za uzinduzi wa Kampeni hiyo leo, iliyofanyika katika Zahanati ya Mtongani.
Diwani Urio kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa Joggingi zote Kata ya Kunduchi, Hamisi Yusuph, kulia.
Diwani wa Kata ya Kunduchi Michael Urio akiwa na Mjumbe wa Kipindupindu Taifa Melone Afrika ambaye alizungumza kwa niaba ya wenzake.
Wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja leo baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo na Diwani Urio, wa tatu kutoka kushoto, na wa pili kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Festo Dugange na kulia kwa Diwani Urio ni Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu.
Comments
Post a Comment