MAJAMBAZI WAVAMIA MGODI NA KUPORA SH. MILIONI 80.
Na
Mwandishi Wetu, Iringa
KUNDI la watu wanaosadikika kuwa ni majambazi
wamevamia mgodi wa machimbo ya dhahabu wa Nyakavangala iliyopo kwenye tarafa ya
Isimani Wilaya ya Iringa na
kuiba fedha zaidi ya sh.Mil.80.
Aidha
watu hao wamefanikiwa kuiba dhahabu zenye uzito wa gramu 490 na simu nne za mkononi
za wafanyabiashara na kujeruhi watu
tisa.
Taarifa
hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya
ya Iringa, Richard Kasesela, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake, alisema majeruhi hao wamepelekeka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Iringa kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Kasesela
alisema alipokea simu kutoka kwa wananchi waliopo kwenye mgodi huo ambao walimueleza
kwamba kuna milio ya bunduki lakini aliwasiliana
na jeshi la polisi na jeshi
hilo lilienda eneo la tukio kwa kuchelewa kutokana na jiografia ya eneo ilivyo
na kukuta majambazi hao wametokomea kusikojulikana.
Alisema
majambazi hao walikuwa na silaha za moto
pamoja na silaha za jadi.
Pia
Kasesela aliwataja majeruhi hao ambao ni Mginya Paulo Gadae(38) mkazi wa
Morogoro ambaye wamemvunja mkono na migu, Bakari maarufu kwa jina la mzee (Beka) na
kusema kuwa mzee huyu wakati anatoka machimboni alikutana na majambazi hao
ambao walimpiga vibaya na hadi sasa yupo kwenye chumba cha uangalizi maalumu
cha wagonjwa mahututi na Sungari Shija (24)mkazi wa geita ambaye aliumizwa
miguu.
Majeruhi
wengine ni Fadhili Naringa Ramadhani mkazi wa Kingonguila Morogoro,Msulwa
Msanga (30) mkazi wa Bariadi , Odrick
Michael(33) mkazi wa Iringa Ipogolo, Kitandu Magula (27) mkazi wa tanga,Daniel
masonja(40) mkazi wa Simiyu na Eliya Mushi ambaye anatoka mkoa wa Kilimanjaro
Moshi.
Kasesela aliwataka wananchi hasa wanaoenda eneo hilo kuacha kutembea na fedha nyingi na badala yake watumie benki.
“Eneo hilo halina mitandao ya simu na hata wakiotupigia simu walitumia njia mbadala kwa kutoka nje ya eneo hilo,” alisema Kasesela na kuongeza .
“Watu hao walitokomea kusikojulikana kwani kule hakuna njia nyinyine ya kutokea na kuingilia na jeshi hadi sasa linaendelea na msako kuhakikisha linawakamata majambazi hao,”
Alisema kuwa kwa sasa waliopo mgodini wameanza na shughuli ya utambuzi na kuongeza kuwa majambazi hao wakati wanavamia na kuumiza walikuwa wanawaambia tuoneshe mtu fulani.
“Hawa watu walienda kwa tageti kubwa sana kwa sababu wakati wameingia kwenye mgodi huo walikuwa wanawaambia tuoneshe mtu fulani.”alisema Kasesela.
Comments
Post a Comment