MATUKIO YA MAOMBEZI NA UPONYAJI KATIKA KANISA LA CHRISTIAN LIFE TEGETA NYUKI.
Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Christian Life, Eliya Peter akitoa huduma ya maombezi kwa mtu mmoja mmoja leo, ambapo maombi ya leo yalikuwa yanasema Nguvu ya Shukrani ni moja ya slaha zote zilizowekwa.
Mchungaji Eliya Peter akiendelea na maombezi ya mtu mmoja mmoja leo.
Mchungaji wa Kanisa hilo akiendelea kutoa huduma ya maombezi kwa mtu mmoja mmoja leo, ikiwa ni siku maalum kwaajili ya maombezi mbalimbali kwenye kanisa hilo, na somo la leo limetoka katika kitabu cha LUKA 17:12-19 na Daniel 6:10.
Waumini waliofika kwenye kanisa hilo kwaajili ya maombezi mbalimbali ya kufunguliwa ikiwamo magojwa pamoja na shida mbalimbali.
Mchungaji wa Kanisa hilo, Edward Mwikonzi akiendelea kutoa huduma ya maombezi ya kufunguliwa kwa wenye shida mbalimbali.
Huduma ya maombezi ikiendelea leo katika Kanisa la Christian Life lililopo Tegeta Nyuki karibu na mabweni ya Shule ya Sekondari ya Canosa, jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Eliya akiendelea kutoa huduma ya maombezi kwa mtu mmoja mmoja leo.
Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo, Eliya akiendelea kumuombea mwananmke huyo aliyetupiwa majini mawili na mama yake mzazi.
Waumini wakiendelea kuomba kwa hisia huku wakisubiri kufikiwa na watumishi wa kanisa hilo kwaajili ya kuombewa.
Mwanamke huyo alilipuka mapepo baada ya watumishi wa Kanisa hilo kumsogerea na kuanza kumuombea.
Huduma ya maombezi ikiendelea katika Kanisa hilo leo na maombezi hayo hufanyika kila siku ya Alhamis kuanzia saa 9:00 asubuhi.
Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo akiendelea kutoa huduma ya maombezi.
Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo akizungumza na waumini leo, hawapo pichani juu ya dada huyo ambaye alifukuzwa nyumbani na wazazi wake baada ya kupata mtoto.
Mchungaji Mkuu Eliya akiendelea kutoa huduma ya maombezi ya kufunguliwa katika vifungo vya mateso mbalimbali kwa mtu mmoja moja .
(PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG), ambao hurusha matukio ya picha za maombezi hayo kila siku ya Alhamis.
Comments
Post a Comment