SITTA ATOA MWEZI MMOJA KWA WAFANYABIASHARA WA BAA NA CLUB.

  Na Enles Mbegalo

MEYA wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta ametoa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wa baa na club kuangalia namna ya ufanyaji wa biashara zao  bila kuleta kero kwa wakazi wa Osyterbay.

Aidha, Sitta alichukua uamuzi huo baada ya malalamiko  ambayo yalitolewa na baadhi ya wananchi wa mtaa huo kwenye mkutano mkuu wa wananchi na wakazi wa eneo hilo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Josho la Mbwa.

Akizungumza na kujibu kero mbalimbali za mtaa huo Sitta alisema biashara ya baa na Club ni biashara ambazo watu wamewekeza na kutoa ajira kwa  vijana ila inapotokea kero kama hizo ni lazima kukaa chini na kuzungumza juu ya suala hilo.

“Natoa mwezi mmoja Mwenyekiti uwaite  wafanyabiashara na kaa nao na mfanye mazungumzo kabla hatujachukua hatua za kisheri,”alisema Sitta na kuongeza

“Mambo haya ni kushauriana kati ya wananchi, Serikali ya Mtaa na wafanyabiashara wenyewe ili waweze kupokea ushauri huu kwa wakazi wa maeneo yaliyokaribu na baa na Club hizi zinazolalamikiwa,”

Hata hivyo wananchi hao walisema baa hizo na club zimekuwa zikikesha  hadi asubuhi na kusababisha kelele kwenye mitaa yao usiku wa manane.
  
Naye Mrakibu wa Polisi, Manispaa ya Kinondoni Abubakari Kunga, akijibu malalamiko ya wananchi hao  juu ya ulinzi na usalama kwenye mtaa huo, aliwaomba wakazi hao kutoa taarifa kwa polisi pale wanapoona kuna watu wasioeleweka kwenye mtaa huo ili kuchukua hatua za kiusalama zaidi.

“Mtaji wa polisi ni taarifa sahihi kutoka kwa wananchi mnapotupa taarifa sahihi ndio inakuwa rahisi sisi kufanya kazi zetu kwani kuna matukio mbalimbali yakiwamo ya uporaji kwa kutumia magari, pikipiki na bajaji yamekuwa yakitokea kwenye mitaa hii mara kwa mara,”alisema na kuongeza

“Naomba muwe na tahadhari kwa matumizi ya simu na mikoba hasa kwa wanawake kwani kunauporaji wa kutumia gari umekuwa ukitokea maeneo haya,”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Zefrin Lubuva alisema mkutano huo ni wa kisheria ambao unawataka kila baada ya miezi mitatu kukaa na kujadili mambo mbalimbali ya mtaa wao na kusikiliza kero za wananchi.

Pia ametoa pongezi kwa wakazi wa eneo hilo kwa kuwa na ushirikiano kwa upande wa mazingira na  imewapelekea mtaa wao kuwa wa kwanza kati ya mitaa 160 na kupokea kombe la Mshindi wa Kwanza wa Usafi wa Mazingira siku Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila mwaka June 5.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Zefrin Lubuva, kushoto akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kazi katika mtaa wake kwa kipindi cha Januari hadi Juni  mwaka huu iliyowasilishwa mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa wananchi na wakazi wa mtaa huo jana, kulia ni Afisa Mtendaji wa Oysterbay Chema Kalembo na Katikati ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta.

Mrakibu wa Polisi, Manispaa ya Kinondoni Abubakari Kunga,akiwaelezea wananchi jinsi walivyojipanga kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mtaa huo.
Mrakibu wa Polisi, Manispaa ya Kinondoni 
Abubakari Kunga, akisaini kitabu cha mahudhurio mara tu baada ya kufika eneo la mkutano.
Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa  Uchaguzi, Jaji Damiani Lubuva  akichangia maoni mbalimbali juu ya kuboresha kwenye mtaa huo ikiwamo kuimarisha ulinzi na usalama.
Wakazi wa mtaa huo wakiendelea kutoa malalamiko ya kero mbalimbali za mtaa huo, ikiwamo kero za baa na club ambazo zimekuwa zikikesha hadi asubuhi na kusababisha kelele kwenye mitaa hiyo na makazi ya watu.
Wakazi wa  mtaa huo wakisikiliza uchangiaji wa mambo mbalimbali ya mtaa wao.
Mmoja wa wakazi wa mtaa huo akielezea jinsi uporaji wa kutumia gari ulivyoibuka kwenye mtaa huo, huku baadhi ya vijana ambao hujificha kwa kisingizio cha kuokota makopo kuingia kwenye nyumba za watu na kuiba.
Mwenyekiti Lubuva akiwa na baadhi ya wakazi wa mtaa wake wakijipongeza kwa mtaa wao kushika nafasi ya kwanza kati ya mitaa 160  na kupokea kombe la Mshindi wa Kwanza wa Usafi wa Mazingira siku Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila mwaka June 5.
Baadhi ya wakazi wakiendelea kufuatilia uwasilishaji wa taarifa za mtaa wao jana.
(PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG).

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.