WAIMBAJI WA INJILI WALIVYOSIFU NA KUABUDU LEO KATIKA KITUO CHA IBAADA CHA MCC.

 Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, Richard Mmari pamoja na mke wake Christina Seme wakiimba nyimbo katika ibaada ya leo ya kituo cha Ibada cha Mliman City Worship Centre (MCC) , jijini Dar es Salaam.
 Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania John Mgina maarufu kama Kichaa wa Yesu akiimba kwenye madhabahu ya MCC leo.
Waumini wakiendelea kuimba katika kipindi cha sifa katika kituo cha ibaada cha MCC leo.
 Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, Dk. Isaya Msangi (MD), akiimba mbele ya madhabahu ya mlimani City, ambapo hufanyika ibaada kila siku ya jumapili kuanzia saa 8:00 hadi 11:00 kwenye ukumbi wa sinema uliopo ndani ya jengo la Mlimani City jijini Dar es Salaam, kituo hicho ambacho kimeanzishwa kwaajili ya kutoa huduma ya maombezi kwa madhehebu yote na hakuna kiingilio.
 Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, wakiongoza kipindi cha siafa leo, katika kituo cha ibaada cha MCC kushoto Christina Seme, katikati ni Jackline Skamwa na kulia ni Slivanus Mumba.
 Waumini wakiendelea kusifu,katika kituo hicho cha ibaada cha MCC leo, katika kipindi cha kusifu na kuabudu.
 Shemasi Dk. Gloria Manyangu (MD) katikati akiwa na waimbaji wa nyimbo za Injili wakiongoza kipindi cha sifa leo katika kituo cha ibaada cha MCC,  ibaada hufanyika kila siku ya jumapili kuanzia saa 8:00 asubuhi na kituo hicho kinasimamiwa na ASKOFU  Mkuu wa Dayosisi Kuu ya Dar es Salaam na Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT), Emmaus Mwamakula.
 Waumini wakiendelea kuimba na kusifu leo katika kituo cha ibaada cha MCC jijini Dar es Salaam na mahubiri ya leo yametolewa na   na  Mwinjilisti Martin Kajituel na kituo hicho kinatumika kwa ibada kila jumapili na kinatumika kwa kutoa ushauri nasaha,maombi ya kufunguliwa,kutoka katika laana na vifungo pamoja na mahubiri.
Waimbaji wa Nyimbo za Injili wakiendelea kuongoza kipindi cha sifa leo katika kituo cha ibaada cha MCC.
Jackline na Shemasi Dk. Grolia wakiendelea kuimba na kusifu katika kituo cha ibaada cha MCC leo, ambapo ibaada hufanyika kila siku ya jumapili katika kituo hicho, na  hufanyika katika ukumbi wa sinema uliopo ndani ya jengo la Mlimani City. 

         (PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG) ambao hurusha matukio ya ibaada hiyo kila siku ya jumapili.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.