MIMEA YA MSITUNI KUTUMIKA KUPANGA UZAZI


Kemikali ya lupeol hupatikana katika mimea ya aloe vera lkwa viwango vidogoKemikali ya lupeol hupatikana katika mimea ya aloe vera kwa viwango vidogo 

 BBC Swahili

Kemikali mbili zinazopatikana katika mimea ya mistuni zinauwezo wa kutengeneza dawa za mpango wa uzazi, ikiwa wanasayansi wangejua wapi wangepata mimea hiyo kwa wingi. 

Kemikali hizo zinapatikana kwenye mizizi ya maua ya dandelion na mmea wa ''thunder god vine'' ambayo umetumika kwa miaka mingi kama dawa za kienyeji.

Sasa watafiti wa Califonia wamesema pia wanaweza kufunga utengenezaji wa mtoto.
Mtaalam wa mbegu za kiume wa Uingereza amesema uzinduzi huo unaweza kuleta njia mpya na ya kudumu ya dawa za mpango wa uzazi kwa wanaume.

Lakini dutu hizo zimepatikana kwa kiwango kidogo kwa mimea lakini gharama ya kupata kemikali hizo kutoka kwa mimea ni ghali sana, kundi moja nchini Marekani limesema.
 Je huenda kemikali kutoka kwa mimea ya msituni ikawa dawa mpya ya kupanga uzazi
Baadhi ya bidhaa zinazotumika kupanga uzazi

Katika majaribio, kemikali kwa jina pristimerin na lupeol zilisimamisha ukuaji wa mtoto kwa kuzuia mbegu ya uzazi kupiga mkia wake na kuogelea katika sehemu ya yai la mwanamke. 

Kemikali hizo zilikuwa zimetekeleza majukumu ya '' aina maalum ya mpira ya kondomu'' muandishi wa utafiti huo aliandika kwenye jarida la Proceedings of the National Academy of Sciences.

Kwa namna nyengine waliziba homoni ya kike ya Progesterone inayosababisha mbegu ya uzazi ya mwanamume kuogelea kwa lazima lakini haikuharibu mbegu hiyo.

Haiui mbegu ya uume wala haina madhara yoyote kwa seli za mbegu za kiumeamesema Polina Lishko ,profesa msaidizi wa seli za baolojia kutoka chuo kikuu cha California , Berkeley. 

Lupeol inapatikana katika mimea kama miembe ,mizizi ya dandelion na Aloe Vera huku pristimerin hutoka kwa mmea wa tripterygium wilfordii unaojulikana pia ''thunder god vine'' na hutumika katika dawa za kienyeji za Uchina.

Watafiti hao wamebaini kwamba kemikali hizo zilifanya kazi kwa kiwango kidogo na hazikuwa na madhara yeyote ikilinganishwa na dawa za mpango wa uzazi zinazotengenezwa ikitumia homoni.

Walihitimisha kwamba kemikali hizo zingeweza kutumika kama za mpango wa dharura wa uzazi kabla na baada ya kujamiana ama dawa za kupanga uzazi maishani kwa kuwekewa dawa hiyo kwenye ngozi. 

Prof Lishko na wenzake wamesema watafanya uchunguzi zaidi kwa nyani ili kubaini jinsi dawa hiyo inavyofanya kazi .

Mbegu za uzazi za nyani ni sawa na za binadamu. Pia wanajaribu kutafuta mbinu za kupata kemikali hizo kwa bei rahisi .

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.