KUMBILAMOTO AWATAKA MADIWANI NA WENYEVITI KUFANYA KAZI KWA BIDII.
Na
Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala ambae pia ni Diwani wa kata ya
Vingunguti Omar Kumbilamoto amewataka Madiwani na wenyeviti wa Serikali za
mitaa (CUF) kufanya kazi kwa bidii na kutoyumbishwa na mgogoro uliopo ndani ya
chama hicho ili kuleta maendeleo kwa wananchi wao.
Pia amesema mgogoro huo ni mdogo sana ndani ya chama hivyo,ni
vyema kuelekeza juhudi zao katika kuwasaidia wananchi kuwatatulia changamoto
zao ambazo wamekua wakikabiliana ndani ya jamii.
Rai hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam leo, wakati alipokua
akitoa msaada kwa wananchi wa kata hiyo ikiwemo mashine ya kuoshea gari pamoja
na jezi za michezo wenye thamani ya sh.mill.1.2 lengo ikiwa lengo ni kuleta
mabadiliko ya haraka kwa wananchi hao.
Kumbilamoto alisema,licha ya mafanikio yaliopatikana kwa kipindi
kifupi lakini pia wanakabiliwa na changamoto ya bati zaidi ya 1300 kwa ajili ya
kuezekea shule zote zilizopo katika kata hiyo ambapo amemuomba Waziri wa nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI) Goerge Simbachawene
kuwatafutia wadau wa kuweza kuwasaidia
"Tatizo la uchakavu wa majengo ndani ya kata yangu imekua
ni tatizo kubwa hususani kipindi hichi cha mvua kwani wanafunzi hulazimika
kuhamishiwa madarasa , na ukiangalia pesa za kodi ya majengo ambazo tunazipata
sisi kama Manispaa ni kidogo zote zinaenda Serikali kuu"alisema
Kumbilamoto.
Aidha aliongeza kuwa,kwa upande wa ukarabati wa barabara
ya Mnyamani Vingunguti iliopo Manispaa ya Ilala, suala hilo lipo katika hatua
ya mwisho kwani wanasubiri idhini ya mkuu wa mkoa kuweza kuruhusiwa mkandarasi
kuanza kazi mara moja.
"Sisi
kama Manispaa ya Ilala tuna uwezo wa kumruhusu mkandarasi huyu lakini awali
mkuu wa mkoa aliwafungia wakandarasi watatu kutokujenga barabara yoyote ndani
ya mkoa wake ambapo na huyu ni miongoni mwa waliofungiwa,"alisema
Kumbilamoto.
NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala ambae pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omar Kumbilamoto, akishirikiana na baadhi ya viongozi wa chama akikabidhi mashine ya maji kwa vijana wa kata ya Vingunguti.
Baadhi ya wananchi ambao walihudhuria kwenye hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment