MAKINDA KUFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA KUJADILI MAENDELEO YA TANZANIA NA KOREA KESHO.
Na Mwandishi Wetu.
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mstaafu
Anne Makinda, anatarajiwa kufungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili maendeleo ya
Tanzania na Korea Kusini na nchi nyingine za Asia kesho jijini Dar es Salaam.
Aidha mkutano huo wa siku tatu utafanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa Budget Entertainmemt Resort uliopo karibu na Hotel ya Bahari
Beach.
Akizungumza na
mwandishi wa blog hii, Rais na Mwazirishi wa Taasisi hiyo isiyokuwa ya Kiserikali ya Chingu Kota Centre, Andrew Dyson Bukuku alisema mkutano huo utajadili maendeleo mbalimbali ikiwamo kwa nini Korea Kusini imepiga hatua
kiuchumi.
Bukuku alitolea mfano wa
miaka ya 1970 na 1980 ya nchi ya Korea ilikuwa tofauti kiuchumi na sasa na nchi hiyo imeweza kupiga hatua kwa
maendeleo.
Alisema kuwa miaka
hiyo Korea Kusini uchumi wake ulikuwa sawa sawa na nchi za Afrika lakini leo
hii nchi hiyo ni moja kati ya nchi zenye uchumi mkubwa dunia.
“Kazi ya Taasisi ya Chingu Kota Centre ni kuandaa matamasha ambayo yanahusu Korea pamoja na nchi zingine za Asia kwa ujumla na katika hayo matamasha yatahusu kujadili maendeleo kwa mfano miaka ya 1970 hadi 1980 Korea Kusini uchumi wake ulikuwa sawa sawa na nchi zenye uchumi mkubwa duniani,”alisema
Bukuku aliongeza kuwa Chingu Kota Centre pia husimamia matamasha ya watu kujifunza maendeleo au mambo mbalimbali ya Kikorea na ni kama daraja la mahusiano kati ya Korea na Tanzania katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano ya Rais John Pombe Magufuli kwa kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini.
Comments
Post a Comment