WANAWAKE WANAHOFIA KUTOA TAARIFA ZA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KWA KUHOFA NDOA ZAO KUVUNJIKA.

 Na Mwandishi Wetu.


MJUMBE wa Halimashauri Kuu ya Taifa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa (MNEC),amesema  wanawake wamekuwa wakihofia kutoa taarifa za unyanyasaji wa kijinsia kwenye familia zao kwa kuhofia ndoa zao kuvunjika.

 Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam, wakati alipokuwa akifungua tamasha la Tunaweza kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya mwanamke, Kata ya Sandali katika viwanja vya Puma.

Magesa alisema endapo hayo mambo yataendelea kufumbiwa macho kwenye familia akinamama  wataendelea kufanyiwa ukatili huo bila kupata msaada wa kisheria.

Aliongeza kuwa unakuta  ndugu wa mme, mme wote wanamfanyia ukatili mwanamke, ila yeye kwa kuhofia  ndoa yake anakaa kimya bila kutoa taaria kwenye vyombo vya kisheria.

“Mtakapofanyiwa ukatili wa aina yoyote ile toeni taarifa kwenye vituo polisi, Serikali za Mitaa, Ustawi wa Jamii, Makanisani, Misikitini na Vituo vya Msaada wa Kisheria ili muweze kusaidiwa  kwa kupewa elimu,”

Pia aliitaka jamii kutumia  fursa hiyo, kwa  kufanya mabadiliko kwenye mitaa na nyumba zao kwani kufanya hivyo ukatili hautokuwepo.
 Aliwasisitiza wanaume kuacha ukatili huo kwani kufanya hivyo ni sawa na kufanya uharifu.
 Aidha amewataka  wanaume  kuwaheshima na kuwadhamini wake zao na kuacha mabavu  ndani ya familia na pia  kuwajibika kwenye familia zao.

“Wanaume tuache unyanyasaji kwa wake zetu kwani kufanya unyanyasaji huu ni uhalifu kama ulivyo uharifu mwingine, tuwaheshimu na kuwadhamini,”alisema na kuongeza

“Kuna kina baba hawawajibike kwenye familia zao ndio maana wamama wengi wamekuwa wakijiunga kwenye vikundi mbalimbali ili waweze kujikwamua na maisha yao,”

 “Kina mama chukueni hatua na msilee manyanyaso ya kwenye familia na tuache kutumila  mila potofu kwa kutunza siri hata unapoona jirani au mtu yeyote anafanyiwa ukatili,”

Pia aliwataka wananchi kusapoti juhudi za Rais John Pombe Magufuli, za kufanya kazi kwani kufanya hivyo hata ukatili wa kijinsia hautofanyika.

Naye, Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali, Anugatha Kayombo alisema Suala la kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake sio la mtu mmoja ni la wote kwa pamoja washirikiane kutoa taarifa katika vituo vya polisi.

 “Wanawake na watoto wanapigwa hadi wanaumizwa lakini watu wamekuwa wagumu kutoa taarifa katika vituo vinavyohusika ili kusaidia matatizo haya kuisha kabisa kwenye jamii ,”alisema

Naye, Mkurugenzi wa Hisia Threatr, Hamis Kussa, kampeni hiyo ambayo ilianza tangu mwezi wa pili mwaka huu ililenga kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanamke ili aweze kujikomboa.

Alisema tamasha hilo  liliandaliwa na kikundi cha Hisia Threatr ikishirikiana na Kituo cha  Msaada Sheria kwa Wanawake (WLAC) kwa lengo la kutokomeza ukatili jinsia kwenye jamii.
Mgeni rasmi akipokea karatasi la wanamabadiliko baada ya kusaini kitabu cha wanamabadiliko jana.

MJUMBE wa Halimashauri Kuu ya Taifa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa (MNEC), katika, kulia Mkurugenzi wa Hisia Kussa na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mambo Leo B, Zuberi Kabumaye wakati walipompokea mgeni rasmi jana kwenye viwanja vya Puma jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye kampeni hizo wakifuatilia burudani mbalimbali za kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia katika viwanja hivyo jana.



 Mkurugenzi wa Hisia Threatr, Hamis Kussa, akiwa na mmoja wa wanakikundi hicho wakiendelea kutoa elimu mbalimbali za ukatili wa kijinsia katika viwanja vya Puma jana.


 Mkurugenzi wa Hisia Threatr, Hamis Kussa, akizungumza na mgeni rasmi mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.


 
 Baadhi ya viongozi waliohudhuria kampeni hizo, Polisi Jamii Kata ya Sandari, Inspecta Athumani Mrisho na Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandari, Engerasia Lyimo.

Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Sandali wakifuatilia burudani mbalimbali za kuelimisha zilizokuwa zikitolewa na kundi la Hisia jana, katika ni  Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali, Anugatha Kayombo,kushoto kwake e ni  Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Engerasia Lyimo na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mambo Leo B, Zuberi Kabumaye.(PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI). 

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.