NBS IMEANZA MAANDALIZI YA UTAFITI WA MATUMIZI YA TUMBAKU KWA WATU WAZIMA NCHINI.
Mtaalam wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima, David
Plotner (kushoto) kutoka shirika la CDC Marekani akijadiliana na maafisa wa
TEHAMA wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Munir Mdee (katikati) na Abdullah Othman
(kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni
jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia
kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Munir Mdee akitoa
mafunzo ya kutumia Dodoso kwa njia ya tablet kwa washiriki wa mafunzo ya
Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima wakati wa mafunzo ya awali ya
utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Utafiti
wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima,Hellen Hillary (kushoto) kwa upande wa
Tanzania Bara akijadiliana na mratibu wa utafiti huo kwa upande wa Tanzania
Zanziar , Nuru Masoud (kulia) wakati wa
mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam.
Meneja wa Takwimu za Jamii, Sylvia Meku (katikati) akiwaelekeza
washiriki wa mafunzo ya awali ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima,
Frank Mapendo (kushoto) na Jocelyne Rwehumbiza (kulia) wakati wa mafunzo ya
awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mwananchi kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam
akijibu maswali kutoka kwa Mtakwimu, Stephen Cosmas wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa
majaribio ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa
Watu wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
Mtakwimu Hellen Mtove wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akimhoji
mwananchi kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati wa majaribio
ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu
wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
(PICHA ZOTE NA VERONICA
KAZIMOTO)]
Comments
Post a Comment