UTAFITI: 'UGONJWA WA SELIMUNDU UNA UHUSIANO NA MALARIA KALI'


https://i.ytimg.com/vi/5F9AzoHD-j8/hqdefault.jpgNA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

TAFITI mbalimbali zinaoendelea kufanyika zinaonesha ugonjwa  wa selimundu unaonekana kuwapo kwa kiwango kikubwa katika sehemu zenye malaria kali ikilinganishwa na maeneo mengine, imeelezwa.

Mratibu wa Mradi wa Kuelimisha Jamii kuhusu ugonjwa wa selimundu nchini (PPE), Promise Mwakale alisema hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza na MTANZANIA kwenye viwanja vya Mbagala Zakheim.

“Watafiti wanafikiria kwamba sickcell ina wiana na malaria kali, hata ukiangalia ramani ya dunia inaonesha wazi sehemu zenye malaria kali ndizo zenye tatizo,” alisema.
 http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2016/11/sickle-cell-300x169.jpg
Alisema watafiti wanafikiri kwamba ugonjwa wa selimundu hulianza kama njia ya mwili kupambana na malaria.

“Kwamba ikiwa seli za damu haziwezi kuishi muda mrefu basi hata wale wadudu wa malaria hawawezi kuishi muda mrefu,” alisema.

Alisema katika Idara ya sickcell, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi kutoka Zanzibar, Pwani, Bagamoyo, Mwanza na Mbeya.

Alisema hata hivyo jamii bado haina uwelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo.

“Wengi hawajui jinsi gani mtu huzaliwa na ugonjwa wa selimundu, upo kwenye vinasaba, ndiyo maana tunahamasisha jamii hasa vijana wajitokeze kupima kujua mapema kama wana vinasaba hivyo au la,” alisema.

Alisema wanawahamasisha wagonjwa waliokwisha gundulika kuwa na ugonjwa huo kuzingatia matibabu na ushauri wanaopewa na wataalamu.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.