ACT- WAZARENDO WAADHIMISHA MIAKA MITATU TANGU KUSAJILIWA KWAKE.

Na Enles Mbegalo

CHAMA cha ACT Wazarendo Mkoa wa Dar es Salaam, kimeadhimisha miaka mitatu tangu kisajiliwe kwa kufungua tawi jipya la Mwanamtoti Kata ya Kijichi  jijini Dar es Salaam.

Aidha katika ufunguzi wa Tawi hilo, liliambatana na ufunguaji wa kongamano lilolenga kujadili sera za Chama hicho na changamoto zake  kwa kipindi hicho cha miaka mitatu.

Akizungumza jana kwenye ufunguzi Kongamano hilo, Mwenyekiti wa ACT -Wazarendo  Mkoa wa Dar es Salaam, Salumu Sudi alisema  pamoja na kongamano hilo wamefanikiwa kupokea wanachama 26 katika uzinduzi wa tawi jipya la Mwanamtoti.
Sudi alisema chama hicho kinalengo la kuongeza wanachama zaidi ya 200,000 kwa mwaka huu ambapo sasa wanawanachama  zaidi ya elfu 78.

“Chama chetu kimetimiza miaka mitatu tangu kisajiliwa na pia  tunaomba mtuamini ili tuweze kupata wananchama wengi kuanzia Serikali za Mitaa, Madiwani na Wabunge,”lisema

Pia alitoapongezi kwa  Rais  Dkt, John Pombe Magufuli kwa kuweza kufanikisha zoezi la watu wenye vyeti feki maana kufanya hivyo  ni kuweka taifa la wasomi na lenye udhubutu.

“Kwenye hili lazima tutoe pongezi  kwa Rais Magufuli hatuwezi kuangalia chama kwenye kusema ukweli tutasema na sehemu ya kukosoa tutakosoa  na huu ndio uzalendo,”

Naye , Katibu Mkoa wa Dar es Salaam, Erinest Kalumna alisema kuna mikakati mbalimbali wamepanga kwa 2017 ikiwamo kusajili wanachama 10,000 kila jimbo  kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi wa Chama cha ACT -WAZARENDO wakiwa wamekaa wakisubiri ufunguzi wa Kongamalo hilo jana katika Ukumbi wa Sawaka jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Salumu Sudi, kulia akiwa na Katibu Mkoa wa Dar es Salaam, Erinest Kalumna jana. 
Baadhi ya wananchama waliohudhulia mkutano huo wakipunga mikono.
 Mwenyekiti Sudi akiwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho.
Wanachama waliokuwa wamekaa meza kuu wakipunga mikono baada ya Mwenyekiti kufungua kongamano hilo jana jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa chama hicho wakiwa katika ukumbi wa mikutano huo, uliofanyika jana.
Katibu wa Chama Erinest Kalumna  hicho akizungumza na wanachama hao jana.
Wanachama waliofika kwenye kongamano hilo wakisubiri ufunguzi na kuaza kujadili changamoto na  mafanikio mbalimbali ya chama hicho.
Mwenyekiti Sudi akiwa na baadhi ya wanachama waliokuwa wamekaa jukwaa la wageni waalikwa.
Mwenyekiti akiwa amekaa na baadhi ya wajumbe wa chama hicho baada ya uzinduzi wa Tawi la  jipya la Mwanamtoti Kata ya Kijichi  jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti akimkabidhi kija huyo kadi ya kujiunga na chama hicho baada ya ufunguzi wa tawi hilo jana.
Wanachama wakiendelea kushangilia baada ya ufunguzi wa kongamano hilo jana.
Mwenyekiti Salumu Sudi akiwa ameshika kadi ya chama hicho kwaajili ya kuanza kuwakabidhi wanachama wapya jana baada ya kuzindua tawi jipya.
Wanachama wakiendelea kushangia sherehe za kutimiza miaka mitatu ya chama chao.
      ( PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI).

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.