DIWANI URIO, KUZINDUA KAMPENI YA WEZESHA MAMA NA MTOTO MPYA WA KUNDUCHI.
Ungana na Diwani Kata ya Kunduchi Michael Urio, katika Kampeni ya Wezesha Mama na
Mtoto Mpya wa Kunduchi, yenye lengo la kuwezesha ujenzi wa wodi ya akina
mama pamoja na chumba cha upasuaji katika Zahanati za Mtongani na Ununio ndani
ya Kata ya Kunduchi.
Uzinduzi wa Kampeni hii utahusisha ufanyaji wa usafi katika Zahanati ya Mtongani siku ya Jumamosi tarehe 3/6/2017.
Karibuni Wote.
Matukio mbalimbali ya Kampeni hii yatatolewa na MAISHA NI HABARI BLOG, siku ya jumamosi.
Comments
Post a Comment