NBS, MFUMUKO WA BEI WA MWEZI HUU HAUJAONGEZEKA.
Na Enles Mbegalo
MFUMUKO wa bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2017 umebakia kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa
mwezi Machi 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi
wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema
inamaanisha kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioisha mwezi Machi 2017
imekuwa sawa.
Pia alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.4
mwezi Aprili 2017 kutoka 102.46 mwezi Aprili 2017.
Kwesigabo aliongeza kuwa,mfumuko wa bei wa bidhaa za
vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia
11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.
“Mfumuko wa
bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2017 umebakia kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa
mwezi uliopita na hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei
za bidhaa za mwezi huu na mwezi ulioisha zilikuwa sawa,”alisema Kwesigabo
Alifafanua kuwa,mfumuko wa bei wa mwezi Aprili 2017
unaopimwa kwa mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.5 ikilinganishwa na ongezeko la
asilimia 1.4 ilivyokuwa mwezi Machi 2017.
“Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.04 mwezi
Aprili 2017 kutoka 108.44 mwezi Machi 2017 kuongezeka kwa fahirisi hizo
kumechangia kuongezeka kwa bei za baadhi ya vyakula,”alisema
Alisema baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia
kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia 4.8, unga wa mahindi
kwa asilimia 7.1, choroko kwa asilimia 6.5, viazi mviringo kwa asilimia 4.0,
nyanya kwa asilimia 7.8, nazi 6.9, mihogo 5.9 na vitunguu 3.5.
Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania alisema uwezo wa sh.100 katika kununua bidhaa
na huduma umefikia sh.91 na senti 71 mwezi Aprili 2017 ikilinganishwa na sh. 92
na seti 21 kwa mwezi Machi mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Takwimu jijini Dar es Salaam leo.
Comments
Post a Comment