BALOZI SEIF MGENI RASMI KILELE CHA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI.
Na Mwinyimvua Nzukwi.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, kesho Mei 3, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yatakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha uandishi wa habari Zanzibar Kilimani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo Shifaa Saidi Hassan kwa vyombo vya habari, imesema maadhimisho ya mwaka huu yameandaliwa kwa pamoja na taasisi nne za habari kwa lengo la kuimarisha umoja miongoni mwao na kutilia mkazo ujumbe wa mwaka huu uliotolewa na umoja wa mataifa.
Shifaa alizitaja baadhi ya shughuli zitakazofanyika wakati wa maadhimisho hayo kuwa pamoja na hutuba ya mgeni rasmi, pia mada mbali mbali zitawasilishwa na kujadiliwa na washiriki wa kongamano hilo.
Alisema ili wadau wa sekta hiyo waweze kutathmini utendaji wa vyombo vya habari, mafanikio yaliyopatikana na changamoto zinazoikabili tasnia ya habari nchini.
“Katika maadhimisho ya mwaka huu, sisi (Baraza la Habari Tanzania – MCT), Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar, Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar na TAMWA (Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania) tumeamua kuiadhimisha pamoja kwa lengo la kuipa nguvu lakini pia kukuza mashirikiano kati yetu kama inavyohimizwa na ujumbe wa mwaka huu”, alisema Shifaa ambae pia ni Ofisa Mwandamizi wa MCT ofisi ya Zanzibar.
Ofisa huyo aliitaja kauli mbiu ya siku hiyo kuwa ni umakini wa fikra, kwa wakati muhimu; nafasi ya vyombo vya habari katika kuendeleza amani, haki na ujumuishwaji inawakumbusha wanahabari na wadau wa sekta hiyo kuzingatia maadili na misingi ya taaluma yao katika utendaji wa kazi zao.

Comments
Post a Comment