MSAMBATAVANGU AACHIWA BAADA YA KUSOTA RUMANDE KWA SIKU SITA.
Na Mwandishi
Wetu, Iringa.
SIKU sita
za aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu kuonja kaa
la moto baada ya jeshi la polisi mkoani hapa kumshikilia na kusota rumande pasipo kupewa
dhamana .
Hata hivyo baada ya kusota kituoni hapo hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa
Iringa imemuachia aliyekuwa mwenyekiti huyo baada ya kukana shitaka
linalomkabili.
Akisoma
shauri hilo wakili wa serikali Alex
Mwita alisema mshitakiwa anashtakiwa kwa kosa la kumshambulia Neema Nyongole
Februari 17 mwaka huu eneo la Kibwabwa m Manispaa ya Iringa kinyume na kifungu cha sheria namba
240 cha mwaka 2002.
Mwita
alisema kuwa shauri hilo limefikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza ili
mshitaiwa aweze kujua shitaka lake na mara baada ya kusomewa shitaka hilo
mshitakiwa alikana kutenda
kosa hilo .
Wakili
Mwita alisema kuwa upelelezi wa shitaka hilo bado unaendelea huku upande wa
utetezi ambao unaongozwa na mawakili wawili ambao Alfred Mwakingwe akisaidia na
Jackson Chaula waliiomba Mahakama hiyo kumuachia kwa dhamana kwa sababu kosa
linalomkabili mtuhumiwa linaruhusu kupewa dhamana.
“Tunaomba
mahakama yako tukufu impe dhamana mshtakiwa kwa sababu kosa lake linaruhusu
kupewa dhamana kwa kuzingatia vigezo na mashariti”alisema Mwakingwe
Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wa Iringa David Ngunyale alisema kuwa
mshitakiwa anaweza kudhaminiwa na watu wawili ambao wanakidhi vigezo
vinavyowekwa na mahakama kwa
kuweka bondi ya tsh Mil moja kwa kila mmoja pamoja na mali isiyoamishika.
Hata hivyo mshitakiwa aliweza kuleta wadhamini wawili
ambao ni Anna Mchami na Frank Andrea wote wakazi wa mkimbizi Manispaa ya Iringa wakiwa na baerua ya
utambulisho pamoja na hati za nyumba.
Hakimu Ngunyale alisema kuwa kwa kuwa mshitakiwa ameleta
wadhamini wawili ambao wamesaini vilelelezo hivyo mahakama imeamuru kumuachia
huru na shauri hilo litatajwa tena Juni 1 mwaka huu.
Hivi
karibuni mwenyekiti huyo alifukuzwa uanachama akiwa ni miongoni mwa makada wa
CCM ambao walifukuzwa uanachama na rais Dk.John Pombe Magufuli mjini Dodoma.
Wengine waliofukuzwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya
wanawake wa CCM (UWT) Sophia
Simba na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho
mkoa wa Dar Es salaam Ramadhani Madibida pamoja na wenyeviti wa mikoa mingine.
Comments
Post a Comment