TIRA YASHAURIWA KUPELEKA ELIMU YA BIMA KWA MADAKTARI.
Na Mwandishi
Wetu, Mafinga.
MAMLAKA ya Kusimamia Shughuli za Bima Nchini
(TIRA) imeshauriwa kupeleka elimu ya bima kwa madaktari walio kazini ili
kuhakikisha watanzania wanaopata ajali kwenye vyombo vya moto wanalipwa fidia
na makampuni ya bima.
Aidha
hiyo ni kinyume na sasa ambapo
waathirika wengi wa ajali za moto hawafaidiki na malipo ya bima kutokana na
kukosa uelewa.
Rai
hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maofisa Tabibu cha Mafinga (COTC),
Israel Mwakasonda wakati Mamlaka ya TIRA
walipotoa elimu ya bima kwa wanafunzi wa chuo hicho mjini hapa.
Alisema
serikali pia inapaswa kuwatazama
madaktari na kuwakatia bima kutokana na hatari nyingi wanazokumbana nazo wakiwa
kazini.
Mwakasonda
alisema kuwa “hili ni nalo ni suala la kuwafikiria na kuwaelimisha ili wapate
bima kwa ajili ya kazi zao kwa sababu kazi za udaktari kwa wakati mwingine zina
madhara yake,” alisema Mwakasonda na kuongeza
“Unaweza
ukajiumiza wakati unahudumia mgonjwa,wagonjwa wengine wanamatatizo ya akili na
mengine mengi na unaweza kupata madhara wakati unamtibu huyo mgonjwa wa akili
na ugonjwa huo ukaambukizwa hata wewe daktari.”
Naye,
Meneja wa TIRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Hilard Maskini, alisema Mamlaka
hiyo inaendelea kutoa elimu ya bima kwa makundi mbalimbali lengo likiwa ni
kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uelewa wa uwapo wa bima na kufaidika na
mafao ya bima mara wanapopata majanga.
Mwakilishi wa Makampuni ya Bima Nyanda za Juu Kusini,
Julius Mayamba, akiwataka abiria kutopanda magari yaliyojaza kupita kiasi.
Maskini
alisema kwa kuanzia wameamua kuanzia na
Maofisa Tabibu ambao ni wanafunzi kwa sababu mara nyingi kwenye fani hizo
wanakutana na watu wengi.
Alisema
mfano watu waliopata ajali lakini kuhusu
kutoa elimu kwa madaktari ambao wapo kwenye hospitali ambao ndio wanakutana na
watu ambao wamepata ajali watakuwa wanawapa elimu hiyo na kuwa endelevu pamoja
na kutoa elimu hiyo kwenye hospitali mbalimbali nchini.
Comments
Post a Comment