MATUKIO MBALIMBALI YA MAOMBEZI KATIKA KANISA LA CHRISTIAN LIFE TEGETA.
Baadhi ya waumini waliofika kwa mara ya kwanza kwenye kanisa hilo, wakijitambulisha leo katika ibaada ya maombezi ambayo hufanyika kila siku ya Alhamis kuanzia saa 10: 00 asubuhi hadi 02:00 mchana.
Waumini waliohudhulia kwenye maombi leo katika kanisa la Christian Life wakisikiliza mahubiri yaliyotolewa na Mchungaji Mkuu wa kanisa hilo,Eliya Peter.
Mmoja wa waumini, wa kanisa hilo, Rehema Mandago ikitoa ushuhuda kwa mambo aliyotendewa na Mungu katika maombi ya Alhamis iliyopita ambapo kanisa hilo lilikuwa na maombezi maalumu kwaajili ya kufunguliwa katika shida mbalimbali kushoto ni Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Eliya Peter.
Waumini wakiendelea kufuatilia mafundisho ya maombi yaliyokuwa yakitolewa na Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Eliya Peter.
Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo, Eliya Peter akimtolea mifano mbalimbali ya kufunguliwa kwa mmoja wa waumini waliofika kwaajili ya kupata huduma za maombezi katika kanisa hilo leo.
Baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wakiendelea kufuatilia mafundisho yanayotolewa na Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo, Eliya Peter leo.
( PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG). ambao watakuwa wanatoa matukio mbalimbali ya siku ya Alhamis kwaajili ya maombezi yanayotolewa katika kanisa hilo, wote mnakaribishwa.
RATIBA ZA IBAADA KATIKA KANISA LA CHRISTIAN LIFE LILILOPO TEGETA NYUKI, ILIPOKUWA HOSTER YA CANOSSA ZAMANI.
SIKU YA ALHAMISI SAA 10:00 HADI 10:30 MAOMBI.
SAA 30:00 HADI 11:15 KUSIFU NA KUABUDU.
SAA 11:15 HADI 12:00 NENO SAA 12:00 MCHANA HADI 2:00 MAOMBI YA KUFUNGULIWA.
NA KILA JUMAPILI IBAADA INAAZA SAA 9:00 ASUBUHI.
Comments
Post a Comment