MWENYEKITI MUNENI ATEMBELEA MAENEO ALIYOTOA AGIZO YABORESHWE NA KUTENGENEZWA BUSTANI ZA MAUA.


 
Muneni akimuonyesha Afisa Utawala wa Kanisa la Mtakatifu Albani, Danny Malonga maeneo ambayo wanatakiwa kuyaboresha na kutengeneza busatani na kutengeneza taa.


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Sea View, Kata ya Kivukoni, Victor Muneni, kushoto  akizungumza na Afisa Utawala wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano(Anglikana), Danny Malonga leo,  wakati alipomtembelea ofisini kwake kwaajili ya kuzungumzia uboreshaji wa mazingira ya maeneo yanayowazunguka kwaajili ya kutengeneza bustani na kupanda maua.

Mwenyekiti Muneni akionyesha bango la Kampuni ya Puma ambalo limejengwa ndani ya hifadhi ya barabara na amefanya  mazungumzo wa uongozi wa kampuni hiyo,  umeafiki kulifanyia marekebisho bango hilo, ambalo lilikuwa likisababisha likihatarisha ajali na kuhatarisha watumiaji wa barabara kuwa katika hali hatarishi.


Mwenyekiti akionyesha eneo hilo lilikuwa kichaka ambacho kilikuwa kimbilio kubwa la vibaka wanaotoka kwenye fukwe za baharini na  kujificha hapo na kufanya uhalifu kwa kutumia bisibisi, visu nyakati za usiku. 


 Huo ni muonekane wa eneo hilo baada ya kufyekwa na sehemu hiyo itaboreshwa kwa kutengeneza bustani ya maua  na kuwekwa taa, ili kupunguza uhalifu uliokuwa ukitokea eneo hilo mara kwa mara.



 Mwenyekiti Muneni akizungumza na wafanyabiashara wa eneo la YMCA  kuhusu uboreshaji wa maeneo hayo, na kuwaondoa wasiwasi kuhusu sehemu ya kufanyia biashara zao.


Mwenyekiti Victor Muneni, akizungumza na Hostel Manager YMCA , Gladness Haule  leo ofisini kwake,  kuhusu changamoto za uboreshaji wa maeneo ya nje ya uzio wa jengo  linalowazunguka kwa kupanda bustani na kuweka taa maeneo hayo.


Gadness akimuonyesha Mwenyekiti maeneo ambayo wameaza kuyaboresha baada ya agizo lake la uboreshaji wa maeneo hayo.


Mfanyabiashara wa viatu, Abdala Chomwi akipanga viatu eneo hilo ambalo linatakiwa kuboreshwa kwa kupandwa maua na amesema kuwa uboreshaji huo wa mazingira utaleta muonekano mzuri wa mazingira hayo. 
    
(PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG)


Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.