MANISPAA YAOMBWA KUSIMAMIA FEDHA ZINAZOTOLEWA KWA WATENDAJI WA MITAA.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Sea View, Kata ya Kivukoni,
Manispaa ya Ilala, Victor Muneni ameiomba Manispaa hiyo kusimamia fedha
zinazotolewa kwa watendaji wa Mitaa kwaajili ya shughuli mbalimbali
za mitaa kwani fedha hizo zimekuwa hazifiki kwenye mitaa hiyo.
Aidha, kitendo hicho kimekuwa kikichangia migogoro kwenye
ofisi za mitaa na kuongeza wimbi la rushwa kwa wananchi wanaohudumiwa katika
ofisi hizo kwani watendaji hawanunui vifaa kwaajili ya matumizi ya ofisi.
Akizungumza
na mwandishi wa blog hii, Muneni alisema watendaji hao wamekuwa wagumu kutoa
fedha hizo, zinazotolewa na Manispaa kwaajili ya matumizi ya stationary
kwa kutotoa fedha hizo zimekuwa zikichochea upokeaji wa rushwa kwa Wenyeviti wa
mitaa kwa fedha hizo zimekuwa hazifiki kwao.
Alisema
Wenyeviti hawana jinsi ya kupata fedha nyingine kwaajili ya kutolea huduma hiyo
ya Stationary ni jukumu la Manispaa.
Aliongeza
kuwa Manispaa husambaza fedha hizo kwenye kata zote kwa matumizi ya
kununua stationary za Ofisi za Mitaa yake lakini watendaji hawatekelezi maagizo
hayo na fedha hizo Manispaa huzitoa kwa maelekezo na matumizi yake.
Alisema
kutokana na fedha hizo kutofika kwenye ofisi hizo inawawia vigumu kutoa
huduma bora na hiyo inachangia wenyeviti kuwatoza fedha wananchi
wakati wanapohitaji kuhudumiwa katika ofisi hizo.
“Naiomba Manispaa isimamie watendaji wa mitaa kwani wamekuwa moja
ya chanzo cha migogoro kwenye ofisi zetu za mitaa kutokana na kutofikisha fedha
hizi,”alisema Muneni na kuongeza.
“Fedha nyingine zinazokuja kwenye uhamasishaji kwenye baadhi ya
mambo ikiwamo Afya haziwafikii walengwa na badala yake zinaliwa na
wanaokabidhiwa,”
Hata hivyo alilalamikia kitendo cha Maafisa Afya kutotembelea mitaa na kukagua hali ya mazingira kwenye mitaa na badala yake wamekuwa wakitembelea maeneo ya biashara tu.
“Maafisa Afya hawasimamii shughuri zao kwenye mitaa na wanatokea baada ya muda mrefu na wanapotokea kwa kipindi hicho huwapa adhabu kali kwa kuwapiga faini wananchi badala ya kutoa elimu juu ya afya ya mazingira kwani wananchi wengi hawana uelewa na sheria ndogo ndogo za Manispaa,”alisema
Aliongeza kuwa maafisa hao wanatakiwa kupita kila wakati kwenye mitaa kwaajili ya kukagua mazingira na kutoa elimu kwa wananchi hivyo wao hawafanyi hivyo.
Comments
Post a Comment