WATUMISHI 134 WAKUTWA NA VYETI VYA KUGUSHI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI.
Enles Mbegalo
WATUMISHI 134 wakutwa na vyeti vya kugushi katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) jijini Dar es Salaam.
Aidha, watumishi hao ni kutoka zaidi ya idara 10
ikiwamo idara ya upasuaji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya
habari leo, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Profesa Lawrence Museru, inasema wafanyakazi hao wamebainika kuwa na
vyeti vya Sekondari vya kugushi.
Taarifa hiyo inasema kuwa, watumishi hao ni kutoka
idara ya Kurugenzi ya Uuguzi watumishi 70, Kurugenzi ya Tiba watumishi 20, Kurugenzi ya
Tiba Shirikishi watumishi 14, Kurugenzi
ya Upasuaji watumishi wanne, Kurugenzi
ya Tehama watumishi 11.
Idara nyingine ni Kurugenzi ya Rasilimali watu, watumishi wawili, Kurugenzi ya Ufundi watumishi watatu, Kurugenzi ya Fedha na Mipango watumishi watatu, JKCI Staff in MNH vote watumishi watatu, Taasisi ya Sayansi Shirikishi za Afya mtumishi mmoja na Vitengo vinavyoripotiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji watumishi watatu.
Pia taarifa hiyo imesema endapo mtu hatoridhika na uamuzi huo kuhusiana na uhalali wa vyeti vyao wametakiwa kukata rufaa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kabla ya tarehe 15 mei mwaka huu, na barua zipitie kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MHN.
Comments
Post a Comment