LUBUVA AANZA UJENZI WA OFISI YA SERIKALI YA MTAA OYSTERBAY.

Na Enles Mbegalo

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Oysterbay, Zefrin Lubuva ameanza rasmi ujenzi wa ofisi ya Serikali ya mtaa wake jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na mwandishi wa blog hii leo, Lubuva alisema ujenzi wa ofisi hiyo utapunguza gharama za kodi ya pango ambayo walikuwa wanalipia kwaajili ya ofisi waliyokuwa wanaitumia.


“Tumeanza ujenzi wa Ofisi hii  na ujenzi umeanza toka juzi na imani yangu hadi mwezi Disemba mwaka huu ofisi hii iwe imeshakamilika,”alisema Lubuva

Lubuva, aliongeza kuwa ofisi hiyo kwa sasa inajengwa kwa nguvu ya ofisi yake, ila kuna baadhi ya wadau walitoa ahidi ya kusaidia ujenzi huo.


“Ujenzi wa awali tumeaza kwa kutumia vyanzo vya ndani vya ofisi na tunatarajia nguvu nyingine kutoka kwa wananchi  pamoja na wadau,”


Alisema ujenzi wa ofisi hiyo mpya itakuwa na vyumba kadhaa ikiwamo Ofisi ya Serikali ya Mtaa, Ofisi ya Afisa Mtendaji, Ukumbi wa mikutano,makitaba ndogo pamoja na Ofisi ya Ulinzi Shirikishi,”alisema


Lubuva, alifafanua kuwa jukumu la ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa ni jukumu la Manispaa ila kutokana na wao kutumia gharama kubwa za pango wameamua kuanza ujenzi huo, ili  fedha zilizokuwa zikitumika kwa  pango za kila mwezi zitumike kwa shughuri nyingine za maendeleo.


“Ofisi tunayotumia sasa tunalipa Sh. 400,000 kwa kila mwezi kwa hiyo ujenzi huu utasaidia fedha hizi kutumika katika shughuri nyingine za maendeleo ya mtaa wetu,”alisema


Mmoja wa Mafundi wanaojenga Ofisi hiyo,Edwin Venance akizungumza na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Osysterbay Zefrin Lubuva leo, wakati alipoenda kuangalia hali ya ujenzi wa ofisi hiyo unavyoendelea.

 Fundi Edwin akiendelea  na ujenzi wa ofisi hiyo leo wakati alipokuwa akizungumza na Mwenyekiti huyo jinsi ya ujenzi wa ofisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Hili ni Kontena ambalo litatumika katika ujenzi wa ofisi hizo.(PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG).

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.